
Na Okuly Julius _ DODOMA
Baraza Kuu la Chama cha Wafanyakazi wa Wakusanya mapato Tanzania (TAREWU), imewahimiza wanachama wake kushiriki kikamilifu katika Uchaguzi Mkuu wa Serikali unaotarajiwa kufanyika mwaka 2025 ili kuchagua viongozi waadilifu, wenye maono na wanaojali maslahi ya wafanyakazi pamoja na usimamizi mzuri wa mapato ya serikali.
Hayo yameelezwa leo Aprili 24,2025 jijini Dodoma na Mwenyekiti wa Chama hicho Alex Muganyizi wakati akifungua Mkutano wa Baraza kuu la nne la chama hicho ,ambopo ameeleza umuhimu wa kushiriki katika uchaguzi.
Muganyizi ameeleza malengo ya kufanyika kwa mikutano ya Mabaraza ya wafanyakazi ikiwemo kuwakumbusha umuhimu wao katika ukuaji na ustawi wa Taasisi.
Katibu wa Chama hicho Michael Marere amesema chama hicho kimekuwa kikimsaidia mwajiri wao katika kukabiliana na changamoto mbalimbali za kiutendaji huku mwenyekiti wa wanawake wa TAREWU Bi.Fatuma Mshuwi amesema bila kufanya uchaguzi huwezi kupata viongozi bora watakao simamia mapato vizuri.
No comments:
Post a Comment