ULEGA AANZA ZIARA MBEYA, APOKELEWA NA RC HOMERA. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, April 21, 2025

ULEGA AANZA ZIARA MBEYA, APOKELEWA NA RC HOMERA.


Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega ameanza ziara ya kikazi mkoani Mbeya na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa huo Dkt. Juma Homera leo tarehe 21 Aprili, 2025.

Akiwa katika Mkoa huo Waziri Ulega atakagua upanuzi wa barabara ya Nsalaga - Ifisi (km 29) inayoendelea kujengwa kwa njia nne Mkoani humo.

Aidha, Waziri Ulega amepata fursa ya kuzungumza na Mkuu wa Mkoa huyo na kumueleza kuwa Serikali itaendelea na utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kimkakati ya barabara Mkoani humo ili kuwezesha kuchochea na kuibua fursa za kiuchumi na biashara katika mkoa huo.

No comments:

Post a Comment