UTUMISHI KUZINGATIA AFYA NA USALAMA WA WATUMISHI MAHALA PA KAZI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, April 15, 2025

UTUMISHI KUZINGATIA AFYA NA USALAMA WA WATUMISHI MAHALA PA KAZI



Na. Veronica Mwafisi-Dodoma


Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imeahidi kuzingatia afya na usalama wa watumishi mahala pa kazi ili kuwa na nguvu kazi itakayowawezesha kufikia malengo la utoaji wa huduma bora kwa umma.

Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi ameyasema hayo wakati akizungumza na watumishi wa ofisi yake katika eneo maalum la mafunzo kwa watumishi wake yanayofanyika kila siku ya Jumatatu Mtumba Jijini Dodoma.

“Ninamshukuru Mkaguzi wa Afya Mwandamizi kutoka OSHA, Dkt. Edwin Senguo kwa kuwasilisha mada kuhusu usalama na afya mahali pa kazi na sisi tunaendelea kuzingatia usalama na afya mahala pa kazi ikiwemo kuboresha miundombinu na mifumo ili kulinda afya za watumishi na kutoa huduma bora kwa wananchi.” amesema Bw. Daudi.

Aidha, amesisitiza watumishi kuendelea kutumia ngazi wakati wa kuingia ofisini kwa kuwa ni sehemu ya mazoezi yanayoimarisha afya.

Kwa upande wake Mkaguzi wa Afya Mwandamizi-OSHA, Dkt. Edwin Senguo amesema Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA) ni chombo cha kusimamia usalama na afya mahala pa kazi kwa kuhakikisha kwamba waajiri wote nchini wanaweka miundo na mifumo inayohakikisha usalama na afya mahala pa kazi vinalindwa.

Dkt. Senguo amesisitiza Ofisi ya Rais-UTUMISHI kusimamia, kuwezesha, kuelimisha na kuhamasisha masuala ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi kwa kuweka mifumo thabiti itakayo zuia ajali, magonjwa na vifo pamoja na uharibifu wa mali ili kupunguza gharama za uendeshaji na kukuza uchumi kwa maslahi ya Taifa.




No comments:

Post a Comment