WAZIRI AWESO ASHUHUDIA UTIAJI SAINI MKATABA WA MRADI WA MAJI NZUGUNI AWAMU YA PILI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, April 15, 2025

WAZIRI AWESO ASHUHUDIA UTIAJI SAINI MKATABA WA MRADI WA MAJI NZUGUNI AWAMU YA PILI




Na Okuly Julius _ DODOMA




Waziri wa Maji JUMA AWESO amesema licha ya ongezeko la watu katika jiji la Dodoma, Wizara hiyo imejipanga kuhakikisha inatatua changamoto ya maji ikiwa ni sehemu ya mkakati wa wizara hiyo.

Aweso ametoa kauli hiyo Jijini Dodoma wakati wa halfa ya utiaji saini mkataba wa ujenzi wa mradi wa maji safi nzuguni awamu ya pili uliofanyika katika ofisi za mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira mkoa wa Dodoma DUWASA ambapo mamlaka hiyo imeingia mkataba na mkandarasi Bahaji Construction work wenye thamani ya shilingi Bilioni 5.6.

Mhe Juma Aweso amesema wizara hiyo haitakuwa kikwazo katika kuhakikisha wakazi wa Dodoma wanapata Maji safi na salama.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira DUWASA Mhandisi Aron Joseph amesema mradi huo utatekelezwa kwa kipindi cha miezi 15 ambapo zaidi ya wananchi laki moja na Elfu ishirini na tatu watanufaika.

Mbunge wa Dodoma Mjini na Waziri wa Madini Anthon Mavunde na Mwenyekiti wa Kamati ya Maji na Mazingira JACKSON KISWAGA waamesema zoezi la utiaji saini huo ni sehemu ya utatuzi wa changamoto ya maji katika jiji la Dodoma kutokana na uhitaji wa huduma hiyo kwa baadhi ya maeneo yenye Mgao.

Itakumbukwa kuwa Eneo la Nzuguni mpaka sasa lina Visima Tisa vilivyokamilika ambavyo vina uwezo wa kuzalisha maji wastani wa lita milioni Ishirini kwa siku ambapo hadi kukamilika kwa awamu ya pili ya mradi huu itasaidia kuongeza hali ya uzalishaji maji kutoka lita milioni 81 hadi 90 kwa siku sawa na ongezeko la asiliami 30 kutoka kwenye chanzo hicho.






No comments:

Post a Comment