Wizara ya Maji yashirikiana na wadau binafsi kufanikisha huduma ya maji - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, April 29, 2025

Wizara ya Maji yashirikiana na wadau binafsi kufanikisha huduma ya maji


Wizara ya Maji inashirikiana na wadau mbalimbali ili kuwa na mfumo madhubiti  wa kusimamia miradi  ya maji hasa kwa maeneo ya vijijini kwa kushirikiana na  Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) 


Kaimu Mkurugenzi wa Sera na Mipango Bw. Alex Tarimo amesema hayo kwa niaba ya  Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji jijini  Dodoma wakati wa kikao kazi na Taasisi ya Kidini chini ya kanisa la Anglikana  kilichojadili mfumo wa utekelezaji wa miradi ya maji inayotekelezwa na Taasisi hiyo katika mikoa ya Lindi, Ruvuma na Mtwara 
kwa ushirikiano na Serikali. 

Lengo la kikao hicho likiwa kuendelea kushirikisha Sekta Binafsi katika  kufikisha huduma endelevu ya maji bila kikwazo kwa wananchi.

Kiongozi wa taasisi hiyo Padre Godfrey Monjera amesema pamoja na jitihada wanazofanya kufanikisha miradi hiyo bado uhitaji wa huduma ya maji upo.

“Sisi kama taasisi ya kidini  tumekuwa tukishughulika na  miradi mbalimbali ikiwemo miradi ya maji,lakini bila kushirikiana vizuri na serikali tusingeona matokeo mazuri” Padre Monjera amesema.

No comments:

Post a Comment