Mkurugenzi wa Vijana,Wizara ya Habari,Vijana na Michezo Zanzibar,Shaibu Ibrahim Muhamed ambaye alikuwa mgeni rasmi akiongea na Wanafunzi na wageni waalikwa
Afisa Msimamizi wa Idara ya Uchenjuaji kutoka mgodi wa Barrick North Mara, Kiugu James akiongea na Wanafunzi katika kongamano hilo.
Mkurugenzi wa Vijana,Wizara ya Habari,Vijana na Michezo Zanzibar,Shaibu Ibrahim Muhamed (kushoto) akibadilishana mawazo na Afisa Msimamizi wa Idara ya Uchenjuaji kutoka mgodi wa Barrick North Mara,Kiugu James wakati wa kongamano hilo.
Wanafunzi kutoka vyuo vikuu vya Zanzibar wakifuatilia mada mbalimbali
Wanafunzi kutoka vyuo vikuu vya Zanzibar wakifuatilia mada mbalimbali
Wanafunzi kutoka vyuo vikuu vya Zanzibar wakifuatilia mada mbalimbali
Wanafunzi kutoka vyuo vikuu vya Zanzibar wakifuatilia mada mbalimbali
Wanafunzi wakipata maelezo katika banda la maonesho la Barrick kwenye kongamano hilo.
Wawakilishi kutoka taasisi zilizofanikisha kongamano hilo katika picha ya pamoja na mgeni rasmi na viongozi wa AIESEC Tanzania.
Baadhi ya wafanyakazi wa Barrick walioshiriki katika kongamano hilo
**
Kampuni ya Barrick nchini imeendelea na dhamira yake ya kuwezesha wanafunzi wa vyuo vikuu ambapo kwa mara nyingine imedhamini na kushiriki kongamano la kuwajengea uwezo wanafunzi wa vyuo Vikuu vya Zanzibar kukabiliana na changamoto mbalimbali wamalizapo masomo yao lililoandaliwa na taasisi ya AIESEC Tanzania na kufanyika katika Chuo Kikuu cha Zanzibar.
Kupitia kongamano hilo, Wanafunzi wa vyuo vikuu vya Zanzibar waliweza kupatiwa mbinu mbalimbali kutoka kwa wataalamu, za kuchangamkia fursa zinazojitokeza ikiwemo za ajira, kujiajiri pia jinsi ya kukabiliana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia yanayoendelea kutokea siku hadi siku yanayoathiri upatikanaji wa ajira.
Wanafunzi pia waliweza kupata nafasi ya kujua shughuli zinazofanywa na kampuni ya Barrick na programu mbalimbali za kijamii zinazotekelezwa na migodi yake ya North Mara, Bulyanhulu na Buzwagi ambao uko katika mchakato wa kufungwa.
Barrick imekuwa ikitoa fursa kwa vijana wa vyuo vikuu mbalimbali nchini kupata mafunzo ya vitendo katika katika migodi yake‘Field attachments’, sambamba na kutoa ajira kwa vijana wa kitanzania wenye weledi wa taaluma mbalimbali katika migodi yake nchini pia imekuwa ikitekeleza programu za kuwainua vijana kiuchumi ili wasibaki nyuma.
Kongamano la AIESEC mwaka huu tayari limefanyika katika vyuo vikuu vilivyopo Dar es Salaam, Morogoro na Dodoma kwa udhamini wa Barrick kwa kushirikiana na wadau wengine.
No comments:
Post a Comment