Na Mwandishi Mbogwe, Geita
Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) imetakiwa kuendelea elimu kwa waathiriwa wa mradi wa ujenzi wa barabara katika halmashauri ya wilaya Mbogwe mkoani Geita zenye jumla ya urefu wa Km. 58 kwa kiwango cha lami zinazotarajiwa kujengwa kupitia mradi wa RISE.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe, Mhe. Sakina Mohamed wakati wa kikao cha pamoja na wataalamu wa TARURA wakishirikiana na Wataalamu Washauri wa Tathmini za Kimazingira na Kijamii, Mpango wa Uhamishaji Watu na Makazi na Usanifu wakati wa zoezi la kuweka wazi viwango vya fidia kwa waathiriwa wa mradi ili kupisha ujenzi wa mradi huo.
"Waathiriwa wa mradi asirukwe hata mmoja, pia hakikisheni nyaraka za zoezi hili zinakuwa sahihi ili kuondoa migogoro wakati wa ujenzi wa barabara ukianza", amesema.
Aidha, amewasihi TARURA mchakato wa kumpata mkandarasi ufanyike haraka ili kazi ya ujenzi ianze mapema kwakuwa wananchi wanasubiri mradi kwa hamu kwani utaongeza kasi ya fursa za kiuchumi na kijamii kwa wananchi.
Mradi huo wa RISE unaogharamiwa na mkopo nafuu toka Benki ya Dunia unatarajiwa kujenga barabara za Masumbwe-Iponya- Nyashimba Km 20, Lulembela-Kiseke- Isebya Km 17 na Mkweni -Nhomolwa-Nyanhwiga Km 21.

No comments:
Post a Comment