KAMATI YA BUNGE  YAIOMBA SERIKALI  KUTOA ELIMU KUHUSU LUMBESA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, May 14, 2025

KAMATI YA BUNGE  YAIOMBA SERIKALI  KUTOA ELIMU KUHUSU LUMBESA



Makamu Mwenyekiti wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda,Biashara,Kilimo na Mifugo Mhe.Mariamu Ditopile, akiwasilisha maoni ya kamati hiyo kwa mwaka wa fedha 2025-2026 leo Mei 14,2025 bungeni jijini Dodoma.

Makamu Mwenyekiti wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda,Biashara,Kilimo na Mifugo Mhe.Mariamu Ditopile, akiwasilisha maoni ya kamati hiyo kwa mwaka wa fedha 2025-2026 leo Mei 14,2025 bungeni jijini Dodoma.


Na.Alex Sonna-DODOMA


KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda,Biashara,Kilimo na Mifugo imeiomba Serikali kujitahidi kutoa elimu kuhusu lumbesa katika maeneo mbalimbali nchini,kwani bado kuna baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu wameendelea kutumia mfumo huo unaowanyonya wakulima na pia unaikosesha Serikali mapato.

Ushauri huo umetolewa leo Mei 14,2025 bungeni Dodoma na Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo,Mhe.Mariamu Ditopile wakati akiwasilisha maoni ya kamati hiyo kwa mwaka wa fedha 2025-2026.

Mhe.Ditopile amesema inashauri Serikali iendelee kutoa elimu kwa wananchi sehemu mbalimbali kuhusu umuhimu wa kutumia vipimo sahihi (mizani) na athari inayopatikana kwa kutumia lumbesa.

“Serikali itoe mwongozo maalum utakaotumiwa na Halmashauri zote nchini ili kuondoa mkanganyiko 17 kuhusu matumizi ya mizani. Aidha, izitake Halmashauri zote zisimamie kwa uwiano ambao utaleta manufaa kwa wakulima,”amesema Mhe.Ditopile

Kuhusu mfumo wa Stakabadhi ghalani,Makamu Mwenyekiti huyo amesema wanaishauri Serikali Kuvisimamia Vyama vya Msingi na kuhakikisha vinawalipa Wakulima fedha zao kwa wakati mara taratibu za mauzo zinapokamilika ili kuondoa migogoro isiyo ya lazima baina ya Serikali na Wananchi.

Pia,Kuhakikisha kuwa tozo na ushuru wa mazao ya Wakulima zinapunguzwa kwa kuwa baadhi zinasababisha kero.
“Marekebisho ya tozo na ushuru yanayolenga kuwapunguzia gharama wakulima yatawapa imani zaidi wakulima hao kwa Serikali yao na hivyo kujitokeza kuuza bidhaa zao kwenye masoko halali badala ya kutumia mifumo isiyo rasmi.

Vilevile Kuendelea kutoa elimu ya uhamasishaji kwa wadau wa mfumo wa stakabadhi ghalani kuhusu kutumia mfumo rasmi kuuza na kununua bidhaa mbalimbali.

No comments:

Post a Comment