KAMATI YA BUNGE YAIOMBA SERIKALI KUIONGEZEA BAJETI WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, May 14, 2025

KAMATI YA BUNGE YAIOMBA SERIKALI KUIONGEZEA BAJETI WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA



Makamu Mwenyekiti wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda,Biashara,Kilimo na Mifugo Mhe.Mariamu Ditopile, akiwasilisha maoni ya kamati hiyo kwa mwaka wa fedha 2025-2026 leo Mei 14,2025 bungeni jijini Dodoma.

Makamu Mwenyekiti wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda,Biashara,Kilimo na Mifugo Mhe.Mariamu Ditopile, akiwasilisha maoni ya kamati hiyo kwa mwaka wa fedha 2025-2026 leo Mei 14,2025 bungeni jijini Dodoma.


Na.Alex Sonna-DODOMA


KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda,Biashara,Kilimo na Mifugo imeiomba Serikali kuiongezea bajeti na kuhakikisha inatolewa yote ya Wizara ya Viwanda na Biashara ili kufanikisha Mapinduzi ya Viwanda.
Ushauri huo umetolewa leo Mei 14,2025 bungeni jijini Dodoma na Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo,Mhe.Mariamu Ditopile wakati akiwasilisha maoni ya kamati hiyo kwa mwaka wa fedha 2025-2026 ambapo amesema Kamati inaona upo umuhimu wa kuendelea kuiongezea fedha zaidi ili iweze kufikia Mapinduzi ya Viwanda yanayokusudiwa.

“Kamati inashauri Serikali kufanya yafuatayo ikiwemo iendelee kuongeza Bajeti ya Wizara hii kila mwaka ili kufanikisha Mapinduzi ya Viwanda na ihakikishe kuwa bajeti inayoidhinishwa na Bunge kila mwaka inatolewa yote kwa wakati ili shughuli zilizopangwa zitekelezeke kikamilifu,”amesema Ditopile

Pia amederma kiwango cha fedha kinachotengwa kwa ajili ya Bodi kupitia bajeti ya Serikali ni kidogo kulingana na kazi kubwa iliyopo.

Aidha, mapato ya ndani hayatoshelezi utekelezaji wa shughuli zilizopo kutokana na sehemu ndogo ya maeneo yanayotekeleza mfumo nchini na idadi ya mazao yanayouzwa kupitia mfumo wa stakabadhi za ghala.

“Kamati inaishauri Serikali kuiongezea fedha Bodi iweze kutanua wigo wa shughuli zake na kuwafikia wananchi wengi zaidi 8 kwa kuwapa elimu kuhusu matumizi ya mfumo, uhifadhi na masoko,”amesema

No comments:

Post a Comment