Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa wa Chama Cha Mapinduzi, Ndg. Rabia Abdalla Hamid, amekutana na kufanya mazungumzo na mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) katika Ukumbi wa Makao Makuu ya CCM, Mjini Dodoma.
Katika kikao hicho, Ndg. Rabia alipata fursa ya kusikiliza changamoto mbalimbali pamoja na kupokea maoni na ushauri kutoka kwa wawakilishi wa makundi mbalimbali ya Asasi za Kiraia walioratibiwa na Mhe Neema Lugangira, Mbunge wa Viti Maalum CCM Kundi la NGOs.
Miongoni mwa waliokutana naye ni pamoja na Baraza la Taifa la NGOs (NACONGO), Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu, wawakilishi wa Machinga, na Chama cha Watu wenye Ulemavu (SHIVYAWATA).
Akizungumza katika kikao hicho, Ndg. Rabia aliwataka wadau wa asasi za kiraia na mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) kuendeleza mshikamano na kushirikiana kwa karibu katika kuunga mkono juhudi za maendeleo. Alisisitiza umuhimu wa kuelekeza nguvu kwa pamoja katika kupambana na changamoto za umasikini, maradhi na ujinga, ili kujenga taifa lenye ustawi na haki kwa wote.
No comments:
Post a Comment