
MKURUGENZI wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania TanTrade,Bi. Latifa Khamis,akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 13,2025 katika ukumbi wa CBE jijini Dodoma kuelekea katika Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara maarufu kama Sabasaba, yatafanyika kuanzia Juni 28 hadi Julai 13, 2025 katika viwanja vya Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.


MKURUGENZI wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania TanTrade,Bi. Latifa Khamis,akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 13,2025 katika ukumbi wa CBE jijini Dodoma kuelekea katika Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara maarufu kama Sabasaba, yatafanyika kuanzia Juni 28 hadi Julai 13, 2025 katika viwanja vya Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Na.Alex Sonna-DODOMA
MKURUGENZI wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania TanTrade,Bi. Latifa Khamis, amesema kuwa maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara maarufu kama Sabasaba, yatafanyika kuanzia Juni 28 hadi Julai 13, 2025 katika viwanja vya Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 13,2025 katika ukumbi wa CBE jijini Dodoma, Bi. Latifa amesema kaulimbiu ya mwaka huu ni: "Maonesho ya Kibiashara ya Kimataifa Sabasaba, Fahari ya Tanzania."
Amesema kuwa katika kuhakikisha maonesho ya mwaka huu yanafanyika kwa mafanikio, TanTrade imeandaa mikakati kadhaa ikiwemo, ukarabati wa majengo na miundombinu katika viwanja vya maonesho, ujenzi wa maeneo ya wazi kwa viwango vya kimataifa.
"Tutaimarisha usafi na huduma za afya kwa kushirikiana na Ofisi ya Mganga Mkuu wa Wilaya ya Temeke, kuongeza idadi ya washiriki na wageni kwa kuandaa burudani mbalimbali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambayo italeta wasanii mbalimbali."amesema Bi.Latifa
Aidha ameeleza kuwa lengo la maonesho hayo ni kutoa fursa kwa wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi kukutana, kubadilishana uzoefu, kutafuta masoko pamoja na kujifunza teknolojia mpya.
Hata hivyo amesema kuwa maonesho haya yamekuwa piani sehemu ya kujifunza kwa wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali nchini.
Kwa upande wa wageni wa kimataifa, mabanda maalum yameandaliwa ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuongeza mapato ya fedha za kigeni. Mabanda hayo ni pamoja na, banda la Jakaya Kikwete, banda la Benjamin Mkapa, banda la Ally Hassan Mwinyi
"Kutakuwa na matumizi ya TEHAMA na tiketi za kuingia zitapatikana kwa njia ya mtandao kupitia mifumo ya YAS na VODACOM."amesema
Maonesho hayo yataambatana na matukio mbalimbali muhimu, yakiwemo,Juni 26, 2025 Mapokezi ya washiriki wa ndani,Juni 27, Mapokezi ya washiriki wa nje ya nchi, Julai 3, Uzinduzi wa programu ya Urithi Wetu, ikiwalenga wanafunzi kutoka vijijini wa mikoa mitano Pwani, Mbeya, Kigoma, Zanzibar Kaskazini na Kusini, Julai 5,Made in Tanzania Day siku ya kuenzi bidhaa na huduma zinazozalishwa nchini, Julai 8, Zanzibar Day, Julai 9, Siku ya Kimataifa ambapo Urusi inatarajiwa kushiriki, Julai 10, Hariana Day
Pia kutakuwa na Kliniki ya Biashara Kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali, kama TBS, Brela, n.k kwa lengo la kuweza kuwapatia huduma washiriki.
No comments:
Post a Comment