WAZIRI JAFO AIPONGEZA WMA KUSIMAMIA KIKAMILIFU UBORA WA BIDHAA ZINAZOZALISHWA VIWANDANI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, May 13, 2025

WAZIRI JAFO AIPONGEZA WMA KUSIMAMIA KIKAMILIFU UBORA WA BIDHAA ZINAZOZALISHWA VIWANDANI

WAZIRI wa Viwanda na Biashara,Mhe.Dkt.Selemani Jafo,akizungumza leo Mei 13,2025,jijini Dodoma,katika Kikao cha Menejimenti ya Wakala wa Vipimo Tanzania (WMA) cha kufanya tathmini ya utekelezaji wa bajeti katika kipindi cha bajeti ya 2024-2025.

Na.Alex Sonna-DODOMA

WAZIRI wa Viwanda na Biashara,Mhe.Dkt.Selemani Jafo,ameupongeza Wakala wa Vipimo (WMA) kwa kuendelea kusimamia kikamilifu ubora wa bidhaa zinazozalishwa viwandani lengo likiwa ni kuhakikisha mtumiaji wa mwisho anapata bidhaa zenye ubora.

Akizungumza leo Mei 13,2025,Jijini Dodoma,katika Kikao cha Menejimenti ya Wakala wa Vipimo Tanzania (WMA) cha kufanya tathmini ya utekelezaji wa bajeti katika kipindi cha bajeti ya 2024-2025 Waziri Jafo amesema WMA imekuwa ikifanya kazi vizuri lakini akawataka kuongeza nguvu kwa wale wanaenda kinyume na sheria za nchi katika uzalishaji wa bidhaa zisizokuwa na ubora.

“Na mimi nawaambia katika suala la haki mimi nitalisimamia hili,katika jambo la kutaka haki za watu tutende haki lazima watu wafuate sheria kwa sababu Nchi inaongozwa kwa sheria,niwapongeze wenye viwanda kwa kuzalisha bidhaa zenye ubora,”amesema Waziri Jafo.

Aidha Waziri Jafo amewaomba watendaji hao kuongeza upendo katika kazi zao kwa kuacha kutengenezeana ajali katika kazi zao kwani lengo ni kuhakikisha kazi zinaenda vizuri kwani kwa kufanya hivyo watapata mafanikio makubwa.

“Hizi nafasi mnazozipata ni kubwa mno,wale wanaokaimu wawe moja kwa moja asifanye kazi kwa mashaka mtu anamashaka anajua kesho analetwa mtu kama mnawapima wapeni hii biashara ya kukaimu sio nzuri,”Amesema Waziri Jafo

Kuhusu utendaji kazi wa WMA,Waziri Jafo amesema : “Ni kwamba wananchi wanapata dhuluma kubwa niwashukuru WMA tangu mmefika hapa nimeona mnavyohangaika kufanya kazi,kwani kulikuwa na malalamiko mengi kuhusu bidhaa zisizokidhi vigezo

Hata hivyo Waziri Jafo amewataka Mameneja hao watumie hekima katika utendaji kazi wao kwa kuangalia pia na suala la utu na wasitumie nguvu na ubabe ila kwa wale wazalishaji wakubwa ni lazima wawaghulikie kwa kufuata haki. “Niliwaambie endelee kukamata kwa sababu lazima tumtetee mlaji lazima tutimize wajibu wetu wengine ni magwiji na wanaushawishi mkubwa muda wote nasema kwa sababu tunasimamia sheria basi tusimamie sheria na tumefikia malengo,”amesema Waziri Jafo

Naye,Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo (WMA), Bw. Alban Kihulla,amesema katika utekelezaji wa bajeti ya 2024-2025 malengo yalikuwa ni kuhakiki vipimo na kikao kilienda vizuri ikiwemo kuhakiki mafuta yanayoingia nchini.

Amesema wamekuwa wakikutana na changamoto mbalimbali na wamekuwa wakizitatua kwa kufauta sheria,kanuni na taratibu ili mhusika asiwe na malalamiko yoyote.

“Ni Habari njema kwa sasa hivi zawalishaji wanazalisha nondo zenye ubora na unene ambao upo sahihi Mheshimiwa Waziri nakushukuru jambo lile jambo hakuwa rahisi,”amesema Bw. Kihulla

Amesema kuna kanuni kuhusu rumbesa aliisaini na kuikataza na wao wameisimamia kwa vitendo kuhakikisha mkulima ananufaika

Kwa upande wake,Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara Wizara ya Viwanda na Biashara Bw.Sempeho Manongi,amesema watahakikisha wanarahisisha ufanyaji wa biashara nchini.

WAZIRI wa Viwanda na Biashara,Mhe.Dkt.Selemani Jafo,akizungumza leo Mei 13,2025,jijini Dodoma,katika Kikao cha Menejimenti ya Wakala wa Vipimo Tanzania (WMA) cha kufanya tathmini ya utekelezaji wa bajeti katika kipindi cha bajeti ya 2024-2025.

WAZIRI wa Viwanda na Biashara,Mhe.Dkt.Selemani Jafo,akizungumza leo Mei 13,2025,jijini Dodoma,katika Kikao cha Menejimenti ya Wakala wa Vipimo Tanzania (WMA) cha kufanya tathmini ya utekelezaji wa bajeti katika kipindi cha bajeti ya 2024-2025.

WAZIRI wa Viwanda na Biashara,Mhe.Dkt.Selemani Jafo,akizungumza leo Mei 13,2025,jijini Dodoma,katika Kikao cha Menejimenti ya Wakala wa Vipimo Tanzania (WMA) cha kufanya tathmini ya utekelezaji wa bajeti katika kipindi cha bajeti ya 2024-2025.

Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara Wizara ya Viwanda na Biashara Bw.Sempeho Manongi,akizungumza wakati wa Kikao cha Menejimenti ya Wakala wa Vipimo Tanzania (WMA) cha kufanya tathmini ya utekelezaji wa bajeti katika kipindi cha bajeti ya 2024-2025 kilichofanyika leo Mei 13,2025 jijini Dodoma.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo (WMA),Bw. Alban Kihulla,akizungumza wakati wa Kikao cha Menejimenti ya Wakala wa Vipimo Tanzania (WMA) cha kufanya tathmini ya utekelezaji wa bajeti katika kipindi cha bajeti ya 2024-2025 kilichofanyika leo Mei 13,2025 jijini Dodoma.

SEHEMU ya Washiriki wakimsikiliza Waziri wa Viwanda na Biashara,Mhe.Dkt.Selemani Jafo,(hayupo pichani) wakati wa Kikao cha Menejimenti ya Wakala wa Vipimo Tanzania (WMA) cha kufanya tathmini ya utekelezaji wa bajeti katika kipindi cha bajeti ya 2024-2025.

WAZIRI wa Viwanda na Biashara,Mhe.Dkt.Selemani Jafo,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua Kikao cha Menejimenti ya Wakala wa Vipimo Tanzania (WMA) cha kufanya tathmini ya utekelezaji wa bajeti katika kipindi cha bajeti ya 2024-2025.

No comments:

Post a Comment