MKUTANO MKUU WA 30 WA CRDB KUIDHINISHA BILIONI 168.9 - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, May 14, 2025

MKUTANO MKUU WA 30 WA CRDB KUIDHINISHA BILIONI 168.9

 


Mkutano Mkuu wa 30 wa wanahisa Benki ya Crdb unatarajiwa kuidhinisha kiasi cha shilingi bilioni 169.8  kwaajili ya Gawio la shilingi 65 kila hisa sawa na ongezeko la asilimia 30 ambapo ni mapendekezo ya bodi ya CRDB.

Akizungumza na vyombo vya habari Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Dkt. Ally Laay, ameeleza kuwa Mkutano Mkuu wa Wanahisa utafanyika kwa siku moja baada ya Semina Maalum ya Wanahisa itakayofanyika lijumaa, tarehe 16 Mei 2025. Ambapo Semina hiyo itafunguliwa rasmi na mgeni rasmi anayetegemewa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango.

Dkt.Laay alisema kuwa benki hiyo imekuwa ikikua siku Hadi siku huku thamani ya hisa katika soko la hisa la dar es salaam likiendelea kukua kwa kasi kutoka shilingi 150 tangu ilipoorodheshwa hadi kufikia shilingi 860 ambapo ni sawa na ukuaji wa asilimia 613.

Kwa Upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB bw.Abdulmajid Nsekela amesema kuwa benki hiyo imekuwa ikitumia mkutano mkuu wa mwaka wa wanahisa kama fursa ya kujitathmini ili kuendelea kukuza na kuboresha huduma zinazotolewa na benki hiyo.

"Mkutano huo unatuwezesha kukuakutana na wawekezaji walioamini na kuwekeza katika benki Yetu,wanaangalia na kutafakari benki Yao ilipotoka na inapoelekea pamoja na hayo tunatumia kama fursa ya kujitathmini na kujitafakari ili kuweza kufikia maono" alisema 

Hata hivyo ameendelea kueleza kuwa Mkutano Mkuu wa Wanahisa unafanyika katika kipindi maalum ambapo Benki ya CRDB inasherehekea miaka 30 tangu kuanzishwa kwake. Maadhimisho haya yanatoa fursa ya kutafakari mafanikio yaliyopatikana katika kipindi hicho, ikiwa ni pamoja na kupanua huduma zake ndani na nje ya nchi, kuimarisha utendaji wa kifedha, na kuendelea kuwa kinara katika kuleta maendeleo kwa wananchi kupitia bidhaa na huduma jumuishi za kifedha.

Pia Nsekela alisema kuwa maandalizi yote ya mkutano mkuu wa 30 wa wanahisa umekamilika kwa asilimia mia moja.

Benki ya CRDB pia ilizindua Ripoti yake ya mwaka 2024 inayoonesha maendeleo makubwa ya kifedha,kiutendaji,na Kijamii yaliyopatikana katika kipindi hicho.





No comments:

Post a Comment