NENDENI MKAITANGAZE SERIKALI. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, May 24, 2025

NENDENI MKAITANGAZE SERIKALI.



Angela Msimbira TAMISEMI


Serikali imewataka Maafisa Habari wa mikoa na halmashauri kote nchini kuhakikisha wanatekeleza kikamilifu jukumu lao la kuhabarisha umma kuhusu utekelezaji wa shughuli za maendeleo zinazofanywa na serikali katika maeneo yao.

Wito huo umetolewa leo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Gerson Msigwa wakati wa akifunga kikao kazi cha Maafisa Habari wa mikoa na halmashauri zote nchini kilichofanyika jijini Dodoma.

Amesisitiza kuwa wananchi wanahitaji taarifa sahihi, kwa wakati, na zenye kueleweka kuhusu miradi ya maendeleo, huduma za kijamii, na mikakati ya serikali ya kuwahudumia.

"Maafisa Habari mnapaswa kuwa sauti ya serikali katika maeneo yenu. Mna wajibu wa kuhakikisha mafanikio ya serikali yanawafikia wananchi, na pia changamoto zinazojitokeza zinaelezwa kwa uhalisia wake," amesema.

Msigwa ameongeza kuwa kutofikisha taarifa kwa wananchi kunapunguza uelewa na ushiriki wao katika utekelezaji wa sera na mipango ya serikali, jambo ambalo linaweza kusababisha upotoshaji au malalamiko yasiyo na msingi.

Serikali imeahidi kuendelea kuwawezesha maafisa habari kwa kuwapatia mafunzo, vifaa na teknolojia ya ikisasa ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.

Vilevile, amewahimiza maafisa habari kushirikiana na vyombo vya habari vya kitaifa na vya jamii katika kueneza taarifa.

“Nendeni mkaitangaze serikali – taifa linawategemea nyinyi kama daraja kati ya serikali na wananchi.”




No comments:

Post a Comment