SERIKALI KUANZISHA MFUMO SHIRIKISHI WA TAKWIMU ZA ELIMU - PROF. MKENDA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, May 16, 2025

SERIKALI KUANZISHA MFUMO SHIRIKISHI WA TAKWIMU ZA ELIMU - PROF. MKENDA



Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ina anzisha mfumo shirikishi wa tafiti za elimu ili kuimarisha Takwimu za elimu nchini.

Akifungua Kongamano la Teknolojia ( Technology Symposium) lililoandaliwa na Kampuni ya _Adapt IT _kwa_ kushirikiana_ na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Mei 15, 2925 jijini Dar es Salaam Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema kuwa Mfumo huo utarahisisha upatikanaji wa taarifa muhimu kwa wadau wa elimu.

Ameongeza kuwa Mfumo huo utawezesha muunganiko na mifumo mingine ya Serikali kama NIDA, RITAOR-TAMISEMI na Uhamiaji kwa urahisi wa taarifa na utoaji huduma.

Ameongeza kuwa mfumo huo utawezesha takwimu zote za elimu kupatikana sehemu moja na kuwasaidia wadau kufuatilia mwenendo wa wanafunzi katika kila hatua ya masomo yao.

Aidha amesema kuwa Wizara itaanza kutoa ripoti ya mwaka yaani (Basic Education Statistics Tanzania) itakayo husisha shule na vyuo vya Serikali na Binafsi.

Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Dkt. Bill Kiwia amesema kongamano hilo linalenga kuboresha mifumo ya ndani ili kuongeza ufanisi wa utoaji huduma kwa wanafunzi na kupunguza gharama kwa Serikali.










No comments:

Post a Comment