ULEGA MSIBANI KWA AWESO PANGANI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, May 12, 2025

ULEGA MSIBANI KWA AWESO PANGANI



Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega leo amefika wilayani Pangani mkoani Tanga kwa Waziri wa Maji Jumaa Aweso kuhani msiba wa mdogo wake Ally Hamidu Aweso aliyefariki ghafla tarehe 9 Mei 2025 mjini Dodoma.

Ulega amempa pole Waziri Aweso kwa kupatwa na msiba huo wa mdogo wake uliotokea wakati Waziri huyo wa Maji alipokuwa akiwasilisha Bajeti ya Wizara yake Bungeni.

Katika tukio hilo la kuhani msiba amefuatana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Balozi Mhandisi Aisha Amour na watendaji wengine kutoka Wizarani na Wakala wa Barabara (TANROADS).

Aidha, Waziri Ulega amefanya ziara ya kikazi mkoani Tanga ya kukagua ujenzi wa barabara ya Tanga - Pangani - Mkwaja - Bagamoyo sehemu ya Tungamaa - Mkwaja - Mkange pamoja na Ujenzi wa Daraja la Pangani.



No comments:

Post a Comment