WABUNGE WAKOSHWA UTULIVU CWT - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, May 24, 2025

WABUNGE WAKOSHWA UTULIVU CWT


Baadhi ya Wabunge ambao wamewahi kuwa Walimu na kushika Nyadhifa mbalimbali katika Chama cha Walimu Tanzania CWT wamewataka wanachama wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kuhakikisha kuwa hali ya utulivu iliyopo kwa sasa ndani ya chama inaendelezwa, hasa wakati huu wa kuelekea katika Mkutano Mkuu wa uchaguzi wa chama hicho.


Wabunge hao ambao ni Mhe Mwl. Magreth Sitta ambaye aliwahi kuwa Rais wa Chama hicho wamesema utulivu wa sasa ndani ya CWT ni tofauti kabisa na hali iliyowahi kushuhudiwa huko nyuma, ambapo migawanyiko na mvutano vilikuwa vikiathiri mwenendo wa chama na maslahi ya walimu. Wameeleza kuwa mabadiliko haya yamefungua njia kwa walimu kushirikiana kwa ufanisi zaidi na Serikali, huku masuala yao yakipewa kipaumbele katika meza za maamuzi


Aidha wabunge hao akiwemo Mhe. Salma Kikwete na Mhe Fatuma Tawdiq wametoa wito kwa wanachama wote wa chama hicho kushiriki uchaguzi kwa utulivu, kwa kufuata kanuni, haki na usawa, bila kuruhusu chokochoko zinazoweza kuvuruga mafanikio yaliyopatikana.


Mkutano Mkuu wa uchaguzi wa CWT unatarajiwa kukutanisha wajumbe kutoka kote nchini, na pamoja na uchaguzi wa viongozi, ajenda nyingine zitahusu maslahi ya walimu, mazingira ya kazi, na nafasi ya walimu katika maendeleo ya taifa.

No comments:

Post a Comment