WAWEKEZAJI SEKTA YA MADINI WAKARIBISHWA MTWARA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Sunday, May 25, 2025

WAWEKEZAJI SEKTA YA MADINI WAKARIBISHWA MTWARA


Na Mwandishi Wetu _ Mtwara


Wawekezaji katika Sekta ya Madini wamekaribishwa kuwekezwa katika mkoa wa Mtwara kutokana na uwepo wa madini ya aina mbalimbali yakiwemo madini mkakati yanayotumika kwenye shughuli za viwanda.


Hayo yamesemwa na Mhandisi wa Migodi Mwandamizi, Michael Mtatiro alipokuwa akizungumza kwa niaba ya Afisa Madini Mkazi wa Mkoa huo, Winnifrida Mrema kupitia mahojiano maalum na wanahabari wanaoandaa kipindi maalum cha kuangazia mafanikio katika Sekta ya Madini.

“Yapo madini mbalimbali yakiwemo yanayotokana na mchanga wa bahari (Heavy mineral sands) yanayohusisha madini ya *Rutile, Titanium, Ilminite na Zircon*” amesema Mtatiro.

Akielezea hali ya makusanyo katika mkoa huo, Mhandisi Mtatiro amesema kuwa, Mkoa wa Mtwara ulipangiwa kukusanya Shilingi Bilioni 9.18 kwa mwaka wa fedha 2024/2025, na kuongeza kuwa hadi sasa wamefanikiwa kukusanya Shilingi Bilioni 7.14 sawa na asilimia 75 ya lengo lililopangwa.

“Tuna imani mpaka mwisho wa mwezi wa sita tutakuwa tumefikia lengo la asilimia 100 la makusanyo,” amesema.

No comments:

Post a Comment