WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YAOMBA SHILINGI BILIONI 359.98 KWA MWAKA 2025/2026 - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, May 19, 2025

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YAOMBA SHILINGI BILIONI 359.98 KWA MWAKA 2025/2026



Wizara ya Maliasili na Utalii imeiomba Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuidhinishiwa jumla ya Shilingi bilioni 359.98 kwa ajili ya kutekeleza malengo na vipaumbele vyake kwa mwaka wa fedha 2025/2026.

Akiwasilisha hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo Bungeni jijini Dodoma, Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Dkt. Pindi Chana, amesema kati ya kiasi hicho, Shilingi bilioni 254.23 zimetengwa kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida, huku Shilingi bilioni 105.75 zikielekezwa kwenye Miradi ya Maendeleo.

Waziri Chana alifafanua kuwa kati ya fedha za Matumizi ya Kawaida, Shilingi bilioni 130.71 ni kwa ajili ya mishahara ya watumishi, na Shilingi bilioni 123.52 ni kwa matumizi mengineyo.

Kwa upande wa Miradi ya Maendeleo, Waziri Chana alisema Shilingi bilioni 32.48 zitatokana na vyanzo vya ndani, huku Shilingi bilioni 73.27 zikitoka katika vyanzo vya nje.

Balozi Chana alisisitiza kuwa rasilimali hizo ni muhimu kwa kuimarisha utoaji wa huduma kwa wananchi pamoja na kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii nchini.

No comments:

Post a Comment