
Na: Mwandishi Wetu
“Dumuni katika maombi, mkikesha na kushukuru”
Nukuu hiyo imetolewa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene kutoka katika Bibilia Takatifu Wakolosai 4:2 wakati aliposhiriki Kongamano lililoandaliwa na Umoja wa Madhehebu ya Dini Pwaga Jimboni Kibakwe-Mpwapwa kwa ajili ya kuwaombea Viongozi wa Serikali na Uchaguzi Mkuu 2025.
Mhe. Simbachawene alisema amani na utulivu katika nchi yetu inatokana na mchango wa Viongozi wa Madhehebu ya Dini kwa kuwaongoza waamini wao kwa kufuata misingi ya amani na upendo iliyoweka Mwenyezi Mungu.
Aidha, aliwashukuru viongozi wa Madhehebu ya Dini kwa kuandaa na kufanya ibada ya kushukuru kama kitabu cha Wakolosai kinavyotukumbusha ikiwa ni ishara ya kuomba tena.
“Mimi pia kwa imani yangu ninaamini kuwa dua na sala kutoka kwa waamini wa madhehebu ya dini zote zinaendelea kuifanya Tanzania kuwa na amani na hivyo Rais, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuendelea kuleta fedha na kufanya maendeleo makubwa Tanzania hususani katika Jimbo la Kibakwe” alisema Mhe. Simbachawene.
Aliongeza kuwa, kila mwanapwaga na Kibakwe kwa jumla anaona maendeleo makubwa katika sekta ya elimu, maji, afya, barabara na umeme hivyo hatunabudi kumpatia tena Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan miaka mitano ili aendelee kuliongoza taifa letu kwa hekima na busara zaidi” alisema Mhe. Simbachawene.
Pia, aliwaomba Viongozi wa Madhebu ya Dini kuendeleea kudumu katika maombi na kushukuru wakati wakiunga mkono jitihada zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha amani na upendo miongoni mwa wananchi inadumu kwa maslahi ya Taifa.





No comments:
Post a Comment