MAANDALIZI YA TATHMINI YA PJT-MMMAM NA MALEZI SUMMIT YAANZA MWANZA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, May 19, 2025

MAANDALIZI YA TATHMINI YA PJT-MMMAM NA MALEZI SUMMIT YAANZA MWANZA



OR – TAMISEMI.


Wizara, taasisi mbalimbali za serikali na binafsi wamekutana leo Mei 19, 2025 jijini Mwanza kwa ajili ya maandalizi ya kikao kazi cha tathimini ya utekelezaji wa programu jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto – PJT-MMMAM kinachotarajiwa kufanyika Mei 21 na 22, 2025.

Kikao hicho kitafuatiwa na mkutano mkubwa wa Malezi Summit utakaofanyika jijini Mwanza Mei 23 na 24, 2025.

Kikao hiki cha utangulizi ni sehemu ya maandalizi ili kufanikisha ushiriki wa maafisa lishe na ustawi wa jamii ikutoka mikoa yote 26 ya Tanzania Bara na wawakilishi kutoka Zanzibar ambao pia watashiriki Malezi Summit ikiwa ni kuelekea tamati ya utekelezaji wa programu hiyo kwa awamu ya kwanza.

Kikao hicho cha tathimini kinatarajiwa kuudhuriwa na washiriki zaidi ya 120 kutoka serikalini na taasasi za kiraia zinazoshughulika na makuzi na malezi ya watoto kutoka katika ngazi za mikoa na halamshauri.






No comments:

Post a Comment