TRA KARIAKOO YAENDELEZA UWAJIBIKAJI KWA JAMII KUELEKEA TUZO ZA RAIS KWA WALIPAKODI NA MIAKA 30 YA TRA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, June 26, 2026

TRA KARIAKOO YAENDELEZA UWAJIBIKAJI KWA JAMII KUELEKEA TUZO ZA RAIS KWA WALIPAKODI NA MIAKA 30 YA TRA

Kariakoo, 26 Juni 2026

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Kariakoo imeendelea na maadhimisho ya miaka 30 ya TRA na maandalizi ya Tuzo za Rais kwa Walipakodi kwa kutekeleza shughuli za uwajibikaji kwa jamii, ambapo leo imekabidhi vifaa tiba katika Hospitali ya Mnazi Mmoja. Msafara huo uliongozwa na Kaimu Meneja wa Mkoa wa Kikodi Kariakoo, Bw. Edson Issanya.

Akizungumza wakati wa makabidhiano, Bw. Issanya alisema, "Tunawashukuru walipakodi kwa mchango wao mkubwa katika mafanikio ya TRA kwa kipindi cha miaka 30. Ushirikiano wao umeiwezesha Serikali kuboresha huduma muhimu za kijamii, huku Tuzo za Rais kwa Walipakodi Bora zikiendelea kutambua na kuthamini walipakodi wanaotekeleza wajibu wao kwa uadilifu."

Kwa niaba ya Hospitali ya Mnazi Mmoja, Daktari Tibezuka Zinga aliishukuru TRA Kariakoo kwa msaada huo, akisema utasaidia kuboresha huduma kwa wagonjwa na kuonesha mchango wa walipakodi katika maendeleo

No comments:

Post a Comment