DUWASA YAAHIDI KUENDELEA KUSIMAMIA USAWA WA KIJINSIA MAHALA PA KAZI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, June 20, 2025

DUWASA YAAHIDI KUENDELEA KUSIMAMIA USAWA WA KIJINSIA MAHALA PA KAZI

Mkurugenzi Mtendaji wa DUWASA, Mhandisi Aron Joseph,wakati akifungua mafunzo ya usawa wa kijinsia kwa watumishi wa mamlaka hiyo leo Juni 20,2025 jijini Dodoma.


Na Mwandishi Wetu, Dodoma


Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA), imeahidi kuendelea kusimamia masuala ya Usawa wa Jinsia Mahali pa kazi na kutekeleza Mwongozo wa Jinsia wa Mamlaka hiyo (DUWASA Gender Strategic Guideline) ili kuweka mazingira salama ya usawa wa kijinsia katika maeneo yote ndani ya taasisi.

Kauli hiyo imetolewa leo Juni 20, 2025 Jijini Dodoma na Mkurugenzi Mtendaji wa DUWASA, Mhandisi Aron Joseph wakati akifungua Mafunzo ya Usawa wa Jinsia kwa Watumishi wa DUWASA.

"Taasisi yetu imekuwa ikizingatia masuala ya usawa wa kijinsia katika shughuli zake za kila siku, kwani zinapotokea nafasi za ajira ulinganifu unazingatiwa kwa vigezo na sifa,"amesema Mha. Joseph.

Aidha, Mha. Joseph ametumia wasaa huo kumtambulisha Mratibu wa masuala ya Jinsia DUWASA Bi. Maria Holela ambapo amesema atawavusha katika masuala yote ya jinsia.

Akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Mratibu wa Mradi wa VEI, Mhandisi Damasen Barthlomew amesema imani yake ni kuwa Mafunzo hayo yatakuwa chachu kubwa kwao na taasisi wakati wa kutoa huduma kwa wananchi.

VEI ni Mradi kutoka nchini Uholanzi ukiwa unaundwa na Mamlaka Saba za nchi hiyo zinazolenga kusaidia Mamlaka za maji Duniani, ikiwemo bara la Afrika ambapo kwa Tanzania imebahatika kupata miradi katika mikoa Minne ambayo ni Dodoma, Mwanza, Arusha na Tanga.





No comments:

Post a Comment