SERIKALI YATOA MFUMO WA RAMANI KUONESHA MAENEO YENYE VIASHIRIA VYA MAJANGA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, June 21, 2025

SERIKALI YATOA MFUMO WA RAMANI KUONESHA MAENEO YENYE VIASHIRIA VYA MAJANGA



Na.Mwandishi Wetu - Dar es Salaam


Serikali imeandaa mfumo wenye ramani inayoonesha maeneo yenye viashiria vya majanga katika mikoa na maeneo yake ili kuweka mikakati ya kukabiliana nayo yanapotokea.

Hayo yalibainishwa jijini Dar es Salaam jana na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu – Sera, Bunge na Uratibu, Dkt. Jim Yonazi, katika kikao kilichohusisha Kamati ya Wataalamu ya Kitaifa ya Usimamizi wa Maafa kilocholenga kujadili Mfumo wa Ramani ya Majanga; Mwongozo wa Utumiaji wa Ramani ya Viatarishi vya majanga nchini; na Mkakati wa Taifa Ugharamiaji wa viatarishi vya Maafa, pamoja na Mwongozo wa Uhawilishaji Fedha za Misaada ya Kibinadamu.

Dkt. Yonazi Alisema, Tanzania inaendelea kuweka mikakati mahsusi kuhakikisha kuwa jamii ya Kitanzania inazuia majanga na inajandaa ipasavyo kukabiliana na majanga yatokanayo na mabadiliko ya tabianchi.

“Serikali imeandaa mfumo mahsusi ambao una ramani mbalimbali zinazoonesha viashiria vya hatari za majanga katika mikoa na maeneo yake. Mfumo huu unasaidia Sekta zote, Mikoa na Halmashauri zote kujipanga na kuweka mikakati ya namna bora ya kukabiliana na vihatarishi vya majanga katika maeneo yao.” Taarifa za vihatarisha katika ramani hiyo, zitasaidia kila mdau katika kupanga na kutekeleza miradi ya maendeleo ikiwemo mipango ya matumizi wa ardhi. alisema.

Aliongeza kuwa: “Mfumo huu utatusaidia kujenga uwezo wa kukabiliana na majanga ndani na nje ya nchi.”

Vilevile, Dkt. Yonazi alisema kikao hicho cha Kamati ya Kitaifa kimepitisha miongozo mbalimbali ya kukabiliana na majanga. Aidha, alieleza miongozo iliyopitishwa itatekelezwa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa kitaifa na kimataifa.

Alieleza kuwa kikao hicho kilihusisha Kamati ya Wataalam ya Kitaifa ya Usimamizi wa Maafa ambao wajumbe wake ni Makatibu Wakuu na Wakuu wa Taasisi zinazohusika zinazohusika na Usimamizi wa Maafa.

Kwa mujibu wa Dkt. Yonazi, lengo ni kuhakikisha kuwa miongozo ya kukabiliana na majanga inapitiwa na kupelekwa katika sekta zote na kusimamiwa ili iweze kutekelezwa

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Profesa. Riziki Shemdoe, alisema ramani hizo zina mchango mkubwa katika kusaidia sekta ya mifugo na uvuvi kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi.

Alibainisha kuwa kupitia matumizi ya ramani hizo, nchi itaweza kupanga kwa ufanisi maeneo ya shughuli za uvuvi na ufugaji kwa kuzingatia maeneo yasiyo na hatari kubwa ya majanga kama ukame, mafuriko au mmomonyoko wa ardhi.

"Ramani hizo zitasaidia kuonesha maeneo yaliyo hatarini kwa mabadiliko ya tabia nchi hivyo kutusaidia katika upangaji wa maeneo kwa ajili ya mifugo, malisho, na miundombinu ya maji.




No comments:

Post a Comment