WAZALISHAJI UMEME MKOANI NJOMBE WATAKIWA KUSHIRIKIANA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, June 21, 2025

WAZALISHAJI UMEME MKOANI NJOMBE WATAKIWA KUSHIRIKIANA

Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Balozi Meja Jenerali Mstaafu, Jacob Kingu (kushoto) akikagua mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia maporomoko ya maji uliopo katika Kijiji cha Masisiwe, Kata ya Ukwama, Wilaya ya Makete Mkoani Njombe unaomilikiwa na Dayosisi ya Kusini Kati ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) kupitia Kituo cha Udiakonia Tandala Juni 20, 2025. Pembeni yake ni Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kusini Kati, Wilson Sanga
Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Balozi Meja Jenerali Mstaafu, Jacob Kingu (katikati) katika picha ya pamoja na viongozi wa Mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia maporomoko ya maji uliopo katika Kijiji cha Masisiwe, Kata ya Ukwama, Wilaya ya Makete Mkoani Njombe unaomilikiwa na Dayosisi ya Kusini Kati ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) kupitia Kituo cha Udiakonia Tandala Juni 20, 2025. Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Teknolojia za Nishati Jadidifu na Mbadala kutoka REA, Mha. Advera Mwijage akifuatiwa na Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kusini Kati, Wilson Sanga. Kulia kwa Balozi Kingu ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Nishati Lutheran (DKK) Investment Ltd inayomiliki mradi huo, Elikana Kitahenga
Muonekano wa Bwawa la maji la kuzalisha umeme la mradi wa Ijangala wa kilowati 360 uliopo katika Kijiji cha Masisiwe, Kata ya Ukwama, Wilaya ya Makete Mkoani Njombe unaomilikiwa na Dayosisi ya Kusini Kati ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) kupitia Kituo cha Udiakonia Tandala.
Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Balozi Meja Jenerali Mstaafu, Jacob Kingu (katikati) akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Nishati Lutheran (DKK) Investment Ltd inayozalisha umeme wa kilowati 360 wa Ijangala, Elikana Kitahenga (kushoto) wakati wa ziara yake kwenye mradi huo unaomilikiwa na Dayosisi ya Kusini Kati ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) kupitia Kituo cha Udiakonia Tandala Mkoani Njombe Juni 20, 2025. Kulia ni Mkurugenzi wa Teknolojia za Nishati Jadidifu na Mbadala kutoka REA, Mha. Advera Mwijage.
Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Balozi Meja Jenerali Mstaafu, Jacob Kingu (kulia) akifurahia jambo na Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kusini Kati, Wilson Sanga (katikati) na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Nishati Lutheran (DKK) Investment Ltd inayozalisha umeme ka kutumia maporomoko ya maji ya Mto Ijangala, Elikana Kitahenga Juni 20, 2025 wakati wa ziara yake ya kukagua mradi huo uliopo katika Kijiji cha Masisiwe, Kata ya Ukwama, Wilaya ya Makete Mkoani Njombe unaomilikiwa na Dayosisi ya Kusini Kati ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) kupitia Kituo cha Udiakonia Tandala.
Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Balozi Meja Jenerali Mstaafu, Jacob Kingu (kushoto)) akielekeza jambo kwa Mkurugenzi wa Teknolojia za Nishati Jadidifu na Mbadala kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mha. Advera Mwijage wakati wa ziara yake ya kukagua Mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia maporomoko ya maji uliopo katika Kijiji cha Masisiwe, Kata ya Ukwama, Wilaya ya Makete Mkoani Njombe unaomilikiwa na Dayosisi ya Kusini Kati ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) kupitia Kituo cha Udiakonia Tandala Juni 20, 2025.


Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Balozi Meja Jenerali Mstaafu, Jacob Kingu ametoa wito kwa waendelezaji wa miradi ya Nishati Jadidifu Mkoani Njombe kufanya kazi kwa kushirikiana ili kuongeza tija kwenye shughuli zao na kuwa mfano bora kwa waendelezaji wa miradi katika mikoa mingine.

Ametoa wito huo Juni 20, 2025 akiwa katika ziara ya kukagua mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia maporomoko ya maji uliopo katika Kijiji cha Masisiwe, Kata ya Ukwama, Wilaya ya Makete Mkoani Njombe unaomilikiwa na Dayosisi ya Kusini Kati ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) kupitia Kituo cha Udiakonia Tandala.

"Kwa wingi wa rasilimali ya maji iliyopo Mkoani hapa ni dhahiri uwezo wa kuzalisha zaidi ya megawati 50 ndani ya Mkoa huu pekee upo, ni suala la nyinyi waendelezaji wa miradi kuunganisha nguvu kwa kufanya kazi kwa kushirikiana na kusaidiana," alisisitiza Balozi Kingu.

Hata hivyo alipongeza kwa jitihada zinazochukuliwa na waendelezaji wa miradi ya kuzalisha umeme katika miradi aliyoitembelea na aliwasisitiza kutoridhika na kiasi kidogo wanachozalisha badala yake wafikirie namna ya kutanua wigo wa uzalishaji ili watanzania waweze kunufaika na umeme wanaozalishwa.

Alisema shughuli nyingi zinahitaji umeme na kwamba Taifa linahitaji kuwa na umeme mwingi wenye kutosheleza ili kuwezesha maendeleo ya kichumi na kijamii hasa ikizingatiwa kuwa umeme ni kichocheo muhimu cha maendeleo na ni nguzo ya uchumi.

Aliwakumbusha kuwa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) upo kwa ajili ya kuwaendeleza hivyo wahakikishe wanafanya kazi kwa karibu na Wakala ili kurahisisha shughuli zao na kufikia malengo waliyojiwekea.

"Serikali kupitia REA ipo kwa ajili yenu, hakikisheni kila hatua mnayopiga mnashirikiana kwa karibu na REA ili miradi iweze kwenda kwa kasi na kuleta tija inayokusidiwa," alisisitiza Balozi.

Kwa upande wake Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kusini Kati, Wilson Sanga aliishukuru Serikali kupitia REA kwa kuchangia uendelezaji wa mradi huo unaozalisha kilowati 360 ambazo zote zinaingizwa katika Gridi ya Taifa kwa makubaliano maalum ya kimkataba na TANESCO.

“Tunaishuru sana Serikali kupitia REA kwa kutuwezesha kutekeleza mradi huu ambao umekuwa na mchango mkubwa kwa jamii inayotuzunguka lakini na Taifa kwa ujumla,” alisema Askofu Sanga.

Naye Mkurugenzi wa Teknolojia za Nishati Jadidifu na Mbadala kutoka REA, Mhandisi Advera Mwijage alisema mradi huo wa Ijangala umenufaika na ruzuku ya Jumla ya Shilingi Milioni 996.

Mbali na uwezeshwaji huo, Mhandisi Mwijage alisema Mwendelezaji mradi amewezeshwa na REA kupata mkopo nafuu wa muda wa miaka 12 uliyotolewa kupitia Benki ya Uwekezaji ya Tanzania (TIB) wenye thamani ya Shilingi Milioni 922 kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa miundombinu ya uzalishaji umeme na utekelezaji wa mradi kwa ujumla.

Mha. Mwijage alisisitiza kuwa milango ya Wakala ipo wazi kwa waendelezaji miradi ya Nishati Jadidifu na kwamba wasisite kuwasiliana na Wakala kwa jambo lolote linalokwamisha uendelezaji wa miradi. Vilevile aliwasisitiza wazalishaji umeme kuhakikisha mazingira yanatunzwa ili kuwa na miradi endelevu.

No comments:

Post a Comment