WIKI YA UTUMISHI WA UMMA KITAIFA DODOMA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, June 17, 2025

WIKI YA UTUMISHI WA UMMA KITAIFA DODOMA


NA. OR - TAMISEMI


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mheshimiwa George Simbachawene (Mb) leo tarehe 17 Juni, 2025 akisaini kitabu cha wageni katika banda la Ofisi ya Rais -TAMISEMI katika Wiki ya Utumishi wa Umma Kitaifa inayofanyika Mkoani Dodoma.

Mhe.Simbachawene ameipongeza Ofisi ya Rais -TAMISEMI kwa kushiriki maonesho hayo amesema, Ofisi ya Rais Utumishi itaendelea kushirikiana na Ofisi ya Rais -TAMISEMI kwa ngazi zote ili kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi.


Kauli mbiu ya maonesho hayo "Himiza matumizi ya Mifumo ya Kidijiti ili kuongeza upatikanaji wa taarifa za kuchagiza uwajibikaji"

No comments:

Post a Comment