Mradi wa Kuimarisha na Kuboresha Elimu ya Awali na Msingi (BOOST), unaotekelezwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), umeongeza kwa kiasi kikubwa fursa za uandikishaji wa wanafunzi wa elimu ya awali kutokana na uboreshaji na ujenzi wa miundombinu mipya ya kujifunzia.
Mratibu wa Mradi wa BOOST mkoa wa Njombe, Bw. Leonard Msendo, amesema kuwa kabla ya kuanza kwa utekelezaji wa mradi huo, uandikishaji wa wanafunzi wa elimu ya awali ulikuwa chini ya asilimia 95.
Ameeleza kuwa mwaka 2023 jumla ya wanafunzi 22,800 waliandikishwa, sawa na asilimia 97.3. Idadi hiyo iliongezeka hadi wanafunzi 24,365 (sawa na 109%) mwaka 2024, na kufikia wanafunzi 20,554 (108%) mwaka 2025.
Aidha, Bw. Msendo ameongeza kuwa uandikishaji wa wanafunzi wa darasa la kwanza pia umeendelea kuimarika. Mwaka 2023 wanafunzi 20,053 waliandikishwa, sawa na asilimia 87. Idadi hiyo ilipanda hadi 24,004 (102%) mwaka 2024, na kufikia wanafunzi 22,840 mwaka 2025, ikiwa ni asilimia 100 ya lengo.
No comments:
Post a Comment