Na Okuly Blog _ DODOMA
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe. Halima Dendegu amesema makusanyo ya mapato ya kodi kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) katika Mkoa wa Singida yameongezeka kwa kutoka Shilingi Bilioni 11.9 mwaka 2021/22 hadi Shilingi Bilioni 30 mwaka 2024/25, sawa na ongezeko la asilimia 152.
Amesema mapato ya ndani ya halmashauri nayo yamepanda kutoka Shilingi Bilioni 14.6 mwaka 2020/21 hadi Shilingi Bilioni 24.8 mwaka 2024/25, sawa na ongezeko la asilimia 69.8.
Dendegu ametoa Takwimu hizo Julai 4, 2025, wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma kuhusu mafanikio ya mkoa huo katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Mkuu huyo wa mkoa amesema mafanikio hayo ni matokeo ya usimamizi madhubuti wa serikali, uhamasishaji wa wananchi kuhusu ulipaji kodi na matumizi ya mifumo ya kidijitali katika ukusanyaji wa mapato.
Akizungumzia maendeleo ya kiuchumi, Mhe. Dendego amesema Pato la Mkoa wa Singida limeongezeka kutoka Shilingi Trilioni 2.709 mwaka 2020/21 hadi Shilingi Trilioni 3.398 mwaka 2024/25
Aidha, pato la wastani kwa kila mwananchi limeongezeka kutoka Shilingi 1,588,604 mwaka 2020/21 hadi Shilingi 1,710,562 mwaka 2024/25.
Ameeleza kuwa katika kipindi cha miaka minne, Mkoa wa Singida umepokea jumla ya Shilingi Trilioni 1.72 kutoka Serikali Kuu, mapato ya ndani na michango ya wadau wa maendeleo kwa ajili ya kugharamia shughuli mbalimbali za uendeshaji na utekelezaji wa miradi ya maendeleo, ambapo kati ya fedha hizo, Serikali Kuu imetoa kiasi cha Shilingi Trilioni 1.055.
Katika sekta ya afya, vituo vya kutolea huduma za afya kuanzia zahanati hadi hospitali vimeongezeka kutoka 203 mwaka 2020/21 hadi 302 mwaka 2024/25. Zahanati zimeongezeka kutoka 173 hadi 246, vituo vya afya kutoka 25 hadi 42, na hospitali za wilaya mpya tano zimejengwa huku hospitali tatu zikifanyiwa ukarabati mkubwa.
Katika sekta ya elimu, shule mpya za msingi 142, shule mpya za sekondari 40, shule saba za amali na vyuo vinne vya VETA vimejengwa au vinaendelea kujengwa. Takribani Shilingi Bilioni 48 zimetumika kutoa elimu bila malipo, huku asilimia 95 ya shule za msingi zikinufaika na huduma ya chakula mashuleni — hali iliyosaidia kupunguza utoro.
Kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022, Mkoa wa Singida una jumla ya wakazi 2,008,058 ambapo wanaume ni 995,703 na wanawake 1,012,355. Kati yao, zaidi ya asilimia 80 wanajihusisha na kilimo na ufugaji kama shughuli kuu za kiuchumi.
Mhe. Dendego amesema mafanikio hayo yanadhihirisha utendaji imara wa serikali katika kuwaletea wananchi maendeleo, huku akisisitiza kuwa juhudi zaidi zitaendelea kufanywa ili kuhakikisha Singida inazidi kuwa mfano wa maendeleo nchini.

No comments:
Post a Comment