
Na. Jeremiah Mbwambo, Gitega- Burundi
Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) Prof. Abel Makubi ameeleza kuwepo kwa madaktari Bingwa kwa siku tano kumeleta manufaa makubwa kwa wananchi wa Burundi
"Kuwepo kwa madaktari bingwa wa BMH katika mkoa wa Gitega kuanzia tarehe 14 hadi 18, Julai 2025, tumewafikia wakazi 1270 wa Gitega nchini Burundi katika magonjwa mbalimbali" alisema Prof. Makubi
Ameongeza kuwa wagonjwa 57 wamefanyiwa upasuaji ambapo, Upasuaji wa mifupa 8, Upasuaji mfumo wa mkojo 20, Upasuaji wa jumla 29.
Aidha, waliopimwa kipimo cha moyo (ECHO for Cardiac) 250, waliopewa rufaa ya kuifuata kambi Bujumbura ni 15 na waliopewa rufaa kwenda BMH ni 8

Kwa upande wake Balozi wa Tanzania nchini Burundi amesema kuwepo kwa kambi hii hapa Burundi kumeimarisha zaidi mahusiano baina ya nchi hizi mbili.
"Mahusiano ya Tanzania na Burundi yapo tangia muda mrefu, hivyo kuja kwa madaktari Bingwa wa BMH kumeendelea kuongeza ukaribu zaidi wa wananchi na madaktari wetu, ninamshukuru Rais wa Tanzania na Rais wa Burundi kwa kuridhia huduma hii kutolewa hapa Burundi" amesema Mhe. Byakanu.
Kambi ya Madaktari Bingwa wa Hospitali ya Benjamin Mkapa imefungwa mkoa wa Gitega, inaenda kuanza mkoa wa Bujumbura kuanzia terehe 21 hadi 25, Julai 2025
No comments:
Post a Comment