
Wanawake wa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) wamekumbushwa kuishi kwa upendo na kukumbuka kwamba jukumu la malezi ya familia ni lao.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Huduma Saidizi Bi. Azimina Mbilinyi wakati wa sherehe ya wanawake iliyowajumuisha wanawake wa TARURA Makao Makuu, Mkoa wa Dodoma na wilaya zake iliyofanyika mwisho mwa wiki jijini Dodoma.
Bi. Mbilinyi alisema kwamba wanawake wanalo jukumu kubwa katika malezi ya watoto na familia kwa ujumla hivyo waepukane na msongo wa mawazo.
Aliongeza kusema kusudi la sherehe hiyo kujipongeza na kuwajengea nguvu mpya wanawake hao kwa kukaa na kusheherekea kwa pamoja.






No comments:
Post a Comment