KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE AMPONGEZA MHE. RAIS SAMIA KAMPENI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Sunday, July 20, 2025

KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE AMPONGEZA MHE. RAIS SAMIA KAMPENI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA


Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Ismail Ali Ussi amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuboresha maisha ya Watanzania kwa kupitia kampeni ya Nishati Safi ya Kupikia.

Ussi ametoa pongezi hizo leo Julai 20, 2025 wilayani Mkalama, Mkoa wa Singida wakati akizindua mradi wa jiko linalotumia nishati safi ya kupikia katika shule ya Sekondari ya Tumuli pamoja na kugawa majiko ya gesi ya Kilogramu 6 yaliyotolewa na Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa bei ya ruzuku ya asilimia 50.

“Mhe. Rais alipoingia madarakani aliahidi kuboresha maisha ya Watanzania pamoja na kulinda rasimali za nchi. Na hili tunaliona kupitia kampeni hii aliyoianzisha na kuisamamia. Kupitia kampeni hii ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia, tunakwenda kuokoa afya pamoja na maisha ya wananchi waliokuwa wakifariki kutokana na matumizi ya nishati zisio safi na salama za kupikia.

Lakini pia kupitia kampeni hii ya nishati safi ya kupikia tunakwenda kuokoa mazingira. Utumiaji wa kuni na mkaa ulikuwa unachangia kukatwa kwa miti hovyo na hivyo kuhatarisha mazingira yetu. Hii inadhihirisha Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan sio tuu anajali kizazi hiki, bali pia anajali kizazi kijacho. Kama watanzania hatuna budi kumuunga Mkono Mhe. Rais kwa kila mmoja wetu kwa kutumia nishati safi ya kupikia,” amesema Kiongozi huyo.

Ussi pia ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama kwa kutenga fedha za ndani zilizowezesha ujenzi wa jiko hilo la kisasa linalotumia nishati safi ya kupikia.

Awali akitoa taarifa kuhusu mradi huo, Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, Mhe. Moses Machali amesema kuwa ujenzi wa jiko hilo linalotumia nishati safi ya kupikia utasaidia kuokoa mazingira kwani awali shule hiyo ilikuwa inatumia kiasi cha shilingi 500,000 kila mwezi kununua kuni kwa ajili ya kupika chakula cha wanafunzi wa kutwa na bweni wanaosoma shuleni hapo.

Katika kuendelea kutekeleza kwa vitendo Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia, Wakala wa Nishati Vijijini (REA) inaendelea na ugawaji wa majiko ya gesi ya Kilogramu 6 kwa bei ya ruzuku ya asilimia 50 kwa wananchi wa Mkoa wa Singida ambapo majiko ya gesi 19,530 yamepangwa na yanaendelea kugaiwa katika Mkoa huo huku Wilaya ya Mkalama majiko 3,255 yameshagaiwa.

Kwa upande wao wananchi wa Wilaya hiyo waliopata mitungi ya gesi wameipongeza REA kwa kutekeleza maono ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa vitendo kwa kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia pamoja na kuwafikishia majiko hayo ya gesi hata wananchi wa vijijini.

“Hatukutegemea kuwa iko siku na sisi tutakuja kutumia gesi kupikia. Tunamshkuru sana Mhe. Rais. Tunaahidi tutakuwa mabalozi kwa wenzetu ili waachane na kutumia kuni na mkaa kupikia ili tutunze mazingira yetu,” amesema Martha Andrea mkazi wa Kijiji cha Tumuli.

















No comments:

Post a Comment