JAMII YAASWA KUWASAIDIA WATOTO WENYE CHANGAMOTO - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, July 30, 2025

JAMII YAASWA KUWASAIDIA WATOTO WENYE CHANGAMOTO



Na WMJJWM- Dar Es Salaam


Jamii imeaswa kuwasaidia Watoto wenye changamoto mbalimbali wakiwemo Watoto yatima na wanaoishi na kufanya kazi mtaani ili waweze kupata Malezi Bora na mahitaji kama Watoto wengine.

Wito huo umetolewa Julai 30, 2025 mkoani Dar Es Salaam na Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. John Jingu alipotembelea Shirika la SOS Village.

Dkt. Jingu amesema Serikali inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imedhamiria kuhakikisha Watoto wenye changamoto mbalimbali wanapatiwa huduma stahiki ili nao wakue na kupata fursa sawa kama Watoto wengine.

Ameongezea kuwa katika kuwasaidia Watoto hao Serikali inashirikiana na wadau mbalimbali likiwemo Shirika la SOS Village ambalo limejikita katika kuwasaidia Watoto wenye changamoto mbalimbali kwa kuwapatia huduma stahiki katika Kijiji chao cha kulelea Watoto.

"Nimetembelea nyumba zenu ambapo mnawalea Watoto nimeona mmeweka mfumo mzuri hasa wa kuwa na wazazi na walezi wa kuwalea watoto hawa ili nao wakue katika Malezi na misingi bora kama watoto wengine wenye wazazi" amesisitiza Dkt. Jingu

Aidha ameyataka Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ambayo yanasaidia Watoto wenye changamoto mbalimbali kwa wakati uliopo kujikita katika kuanzia miradi itakayoweza kusaidia kuendesha na kuwa uendelevu wa shughuli za kusaidia Ustawi wa Watoto wenye changamoto mbalimbali.

Kwa upande wake Naibu Mkurugenzi wa Shirika la SOS Village Dorothy Ndege amesema Shirika hilo litaendelea kushirikiana na Serikali na wadau wengine katika kuhakikisha Watoto wenye changamoto mbalimbali wakiwemo Watoto yatima na wanaoishi










na kufanya kazi mtaani wanapata huduma stahiki.

No comments:

Post a Comment