LINDI YAJIVUNIA MCHANGO WA NGOs KATIKA MAENDELEO - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, July 10, 2025

LINDI YAJIVUNIA MCHANGO WA NGOs KATIKA MAENDELEO



Na. WMJJWM-LINDI


Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Telack amesema Serikali inatambua mchango wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali katika kuleta maendeleo kwa wananchi.

Hayo yamesemwa Julai 10, 2025 na Mkuu wa Wilaya ya Lindi Mhe. Victoria Mwanziva kwa niaba ya Mkoa huo wakati akifungua Jukwaa la Mwaka la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali mkoani Lindi.

Mhe. Victoria amesema Serikali inatambua mchango wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali katika kuwahudumia wananchi katika maeneo mbalimbali


"Niseme kuwa NGOs ni mkono wa pili wa Serikali katika kuleta maendeleo kwa jamii hivyo tutaendelea kuweka mazingira wezeshi ya kufanya kazi zenu na kutekeleza miradi mbalimbali." amesema Mhe. Victoria

Ameongeza kuwa Mashirika hayo yanatakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia Sheria na taratibu zilizopo ikiwemo kutekeleza matwakwa Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kwa kuhakikisha yanawasilisha taarifa zake za robo Mwaka na Mwaka pamoja mikataba ya kifedha katika utekelezaji wa miradi mbalimbali.

"Tufuate Sheria na Kanuni zilizopo katika utekelezaji wa majukumu yetu haswa katika kufanya kazi na Mamlaka ambazo tunafanya kazi zetu mfano Afya, Maji, Elimu, Mazingira na Sekta zingine ili tuwe na uratibu mzuri wa utekelezaji wa miradi" amesisitiza Mhe. Victoria

Kwa upande wake Mwakilishi wa Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Fransisca Mwendesha amesema Serikali inatambua kazi kubwa ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali katika kuwahudumia wananchi ila ameyataka Mashirika hayo kuendelea kuzingatia Sheria taratibu zilizopo ili waweze kuwa katika mazingira mazuri ya Utekelezaji wa majukumu yao.


Naye Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NACoNGO) Jasper Makala amesema Baraza hilo linaendelea kuwa kiungo muhimu katika ya Sekta ya NGOs na Serikali,hivyo amewaomba Mashirika hayo kuendelea kuzingatia Sheria taratibu zilizopo katika utekelezaji wa majukumu ili kutimiza malengo ya Shirika na Serikali kwa ujumla.

Majukwaa ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kuanzia ngazi ya Halmashauri mikoa na Taifa yanaongozwa na Kaulimbiu isemayo: Tathmini ya Mchango wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali katika Maendeleo ya Taifa 2020/2021-2024/2025; Mafaniko, Changamoto, Fursa na Matarajio.






No comments:

Post a Comment