Mwenyekiti Mstaafu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, ameibuka kwa mara ya kwanza kwenye hafla ya kitaifa baada ya ukimya wa muda mrefu, akihudhuria uzinduzi wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 uliofanyika jijini Dodoma.
Akizungumza mara baada ya hafla hiyo, Mbowe alisema alialikwa rasmi na Waziri wa Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo, na aliona ni muhimu kushiriki kutokana na mchango mkubwa uliotolewa na CHADEMA katika maandalizi ya Dira hiyo.
Mbowe alitaja sababu tatu zilizomsukuma kuhudhuria hafla hiyo, kuwa ni pamoja na Kushiriki mchakato wa kitaifa wenye umuhimu mkubwa kwa maendeleo ya vizazi vijavyo lakini pia Kuheshimu mwaliko rasmi wa serikali, jambo alilosema linaonesha namna ushirikiano unavyoweza kujengwa licha ya tofauti za kisiasa.
Uzinduzi wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 umefanyika leo Julai 17, 2025, ukiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali, wanasiasa, wanataaluma na wadau wa maendeleo.
No comments:
Post a Comment