Na Neema Mbuja, Tanga
Imeelezwa kuwa mradi wa ujenzi wa bomba la Mafuta ghafi la Afrika Mashariki -EACOP hauna athari za kimazingira kutokana na Serikali kuweka Sera nzuri na Teknolojia rafiki kwa mazingira ili kulinda Bayoanuai wakati wa upitishaji wa bomba la Mradi chini ya mto zigi
Hayo yameelezwa na msimamizi wa mradi wa ujenzi wa bomba kuvuka mto Sigi kinachojumuisha ulazaji wa bomba na uchorongaji kwa ajili ya kuvusha bomba chini ya mto Mhandisi Thomas Mhando, wakati alipokuwa akielezea maendeleo ya mradi kwenye eneo hilo,sambamba na kuhakikisha mazingira yanalindwa kipindi chote cha kusimika bomba hilo

Amesema wakati wa utekelezaji wa shughuli za ujenzi wa bomba linalopita chini ya mto, suala la uhifadhi wa mazingira limepewa kipaumbele cha hali ya juu sambamba na kutoa elimu kwa wananchi juu ya utunzaji wa vyanzo vya maji hasa cha mto Zigi ,kwani ndio tegemeo kwa wananchi wa Tanga na mradi wa EACOP kwa ujumla,ambacho kinahudumia takribani watu 26,552 ambao wanapatiwa maji na mamlaka ya maji Tanga uwasa.
Ameongeza kuwa, wakati wa utekelezaji wa mradi kupeleka maji EACOP, walikubaliana kuwawezesha pia wananchi wa vijiji saba vilivyoko karibu na maeneo ya utekelezaji wa mradi kwa kuhakikisha wanapatiwa maji chini ya mradi wa makubaliano ambapo Jumla ya shilingi Bilioni 2.728 zilitolewa na EACOP kutekeleza mradi wa maji ili wananchi pia wapate maji.
Awali akizungumza kwenye eneo la utekelezaji wa mradi huo mratibu wa kitaifa wa mradi kutoka TPDC Asiadi Mrutu amesema, kwa sasa uvushaji wa bomba kwenye mto Sigi unaendelea vizuri na umefikia asilimia 63 na unatarajiwa kukamilika mwezi Novemba, 2025 na ameishukuru NEMC kwa kusimamia suala la mazingira kwenye mradi huo kwa kuhakikisha wanatembelea Mara kwa mara ili kuona kazi inavyoendelea.
Kwa upande wake, Mhandisi kutoka kitengo cha Miradi Tanga Uwasa Mhandisi Aaron Chanimbaga ameishukuru EACOP kwa kuhakikisha wananchi wanafikiwa na huduma ya maji saa 24 tofauti na ilivyokuwa awali na bomba hilo Lina uwezo wa kutoa lita za ujazo milioni moja na laki saba kwa siku na linahudumia wananchi wa Chongoleani, Ndaoya, Putini, Elani,Mleni, Mabokweni,na Kibafuti.
Ameishukuru Serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa ujio wa mradi wa bomba la Mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani mkoa wa Tanga na kueleza kuwa umeleta mabadiliko ya Kiuchumi kwa mkoa wa Tanga

No comments:
Post a Comment