Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa (wa pili kutoka kulia) akikabidhi hundi ya msaada wa shilingi milioni 20 kwa viongozi wa kikundi cha Busindi Asali zilizotolewa na Taasisi ya kimataifa ya Nos Vies en Partage (NVeP) kushoto ni Mwanzilishi wa taasisi hiyo ambaye pia ni Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Barrick Mining Corporation, Mark Bristow,hafla ya kukabidhi msaada huo ilifanyika katika mgodi wa Bulyanhulu.
Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Barrick Mining Corporation, Mark Bristow akishirikiana na Naibu Waziri wa Madini,Dkt. Steven Kiruswa kukabidhi hundi ya msaada wa shilingi milioni 20 kwa viongozi wa taasisi ya St. Justin Foundation katika hafla iliyofanyika katika mgodi wa Bulyanhulu.
Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Barrick Mining Corporation, Mark Bristow akishirikiana na Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa kukabidhi hundi ya msaada wa shilingi milioni 20 kwa kiongozi wa taasisi ya Sustainable Planet Foundation katika hafla iliyofanyika katika mgodi wa Bulyanhulu
Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Barrick Mining Corporation, Mark Bristow akishirikiana na Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa kukabidhi hundi ya msaada wa shilingi milioni 20 kwa viongozi wa kikundi cha Nazareth katika hafla iliyofanyika katika mgodi wa Bulyanhulu.
***
Taasisi ya kimataifa ya Nos Vies en Partage (NVeP), kwa kushirikiana na kampuni ya Barrick, imetoa msaada wa shilingi milioni 80 kwa mashirika manne yasiyo ya kiserikali kutoka mikoa ya Shinyanga, Mara, Pwani na Dodoma kwa ajili ya kukabilianana changamoto mbalimbali za kijamii.
Mashirika yaliyonufaika na msaada huo kila moja likiwa limepata shilingi milioni 20 ni Busindi Asali, St.Justin Foundation,Nazareti Group-Nkulabi na Sustainable Planet Foundation.
Msaada huo umetokana na sehemu ya fedha zilizotolewa na taasisi ya kimataifa ya Nos Vies en Partage (NVeP), iliyoanzishwa na inayofadhiliwa na Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Barrick Mining Corporation, Mark Bristow, kwa ajili ya kusaidia makundi maalum kama vile Wanawake, watoto na makundi mengine yenye uhitaji yasiofaidika na ukuaji wa kiuchumi barani Afrika.
Kila robo ya mwaka taasisi ya NVeP, imeweza kutoa misaada yenye tija na manufaa ya moja kwa moja kwenye jamii mbalimbali zenye uhitaji barani Afrika na kufikia sasa zaidi ya mashirika 35 yasiyo ya Kiserikali na taasisi za kijamii nchini yamepatiwa msaada huo na tayari umeleta mabadiliko chanya katika jamii hususani katika sekta ya elimu, afya kwa Wanawake na watoto , utunzaji wa Mazingira na kuendeleza miradi midogo midogo ya kujikwamua kimaisha.
Akiongea wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wakati wa ziara yake ya kikazi nchini iliyofanyika kwenye mgodi wa Bulyanhulu, Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Barrick Mining Corporation, Mark Bristow, amesema kuwa taasisi ya ya NVeP, itaendelea kusaidia mashirika yasiyo ya kiserikali na taasisi ambazo zinatoa huduma kwa jamii kuendana na malengo ya taasisi hiyo sambamba na kuleta mabadiliko chanya katika jamii na kuwataka wanufaika kutumia fedha hizo kwa malengo yaliyokusudiwa
Akizungumza kwa niaba ya wanufaika wenzake, Meneja wa taasisi ya St. Justin Foundation lenye makao mkoani Mara, Juma Songo, ameshukuru NveP kwa msaada huo na kueleza kuwa utasaidia kukabiliana na changamoto za kijamii kupitia taasisi hizo.
Naye katibu wa kikundi cha Busindi Asali,Tatu Lukuba, amesema kuwa msaada huo kwao ni mkubwa na utawawezesha kupanua mradi wao wa ufugaji wa nyuki na kuwezesha wanakikundi kujikwamua kimaisha na kuboresha maisha yao na familia zao.
"Waswahili walisema akufaaye kwa dhiki ni rafiki,tunashukuru msada huu mkubwa tulioupata kutoka Nvep na Barrick" amesema.
No comments:
Post a Comment