
Mkurugenzi wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Fredrick Salukele
akizungumza wakati akifungua semina ya ushirikiano Kati ya Tanzania na Idara ya Elimu ya Jamhuri ya China iliyofanyika
leo Julai 11, 2025 katika ukumbi wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Elimu ya Mkoa wa Sichuan, Jamhuri ya Watu wa China, Prof. Yu Xiaoqi akizungumza wakati wa semina ya ushirikiano Kati ya Tanzania na Idara ya Elimu ya Jamhuri ya China iliyofanyika leo Julai 11, 2025 katika ukumbi wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Bodi Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) Bi. Bernadetta Ndunguru.
akizungumza wakati wa semina ya ushirikiano Kati ya Tanzania na Idara ya Elimu ya Jamhuri ya China iliyofanyika leo Julai 11, 2025 katika ukumbi wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) Dar es Salaam.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) Dkt. Mwajuma Lingwanda akizungumza wakati wa semina ya ushirikiano Kati ya Tanzania na Idara ya Elimu ya Jamhuri ya China iliyofanyika leo Julai 11, 2025 katika ukumbi wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) Dar es Salaam.

Rais wa Chuo Kikuu cha Dalian, Kitengo cha Uchapishaji Dkt. Su Kezhi akizungumza wakati wa semina ya ushirikiano Kati ya Tanzania na Idara ya Elimu ya Jamhuri ya China iliyofanyika leo Julai 11, 2025 katika ukumbi wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) Dar es Salaam.
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) kwa kushirikiana na Wakuu wa Taasisi za Elimu ya Kati wameahidi kushirikiana na Idara ya Elimu ya Jamhuri ya Watu wa China katika kuandaa mitaala ya elimu inayolenga kutoa ujuzi unaoendana na mahitaji ya soko la ajira na mahitaji ya dunia ya sasa.
Akizungumza leo, Julai 11, 2025, jijini Dar es Salaam wakati akifungua semina ya tano ya ushirikiano kati ya Tanzania na Idara ya Elimu ya Jamhuri ya Watu wa China kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mkurugenzi wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi, Dkt. Fredrick Salukele, amesema kuwa semina hiyo imelenga kuboresha mafunzo ya elimu ya ufundi stadi nchini ili kuhakikisha sekta ya elimu inaendelea kusonga mbele kwa ufanisi.
Dkt. Salukele amesema kuwa semina hiyo imeshirikisha wakuu wa taasisi za elimu ya kati, menejimenti ya NACTVET, Chuo cha Ufundi Stadi (VETA), ambapo kwa pamoja wamekubaliana kushirikiana na Jamhuri ya Watu wa China ili kuendana na sera ya sasa inayolenga elimu yenye ujuzi na hivyo kuhakikisha malengo yanafikiwa.
"Dunia ya sasa inaendeshwa kwa kutumia akili mnemba, na wenzetu kutoka China wameahidi kuendelea kushirikiana nasi katika kutengeneza vitabu vya kujifunzia na kufundishia kwa ajili ya wanafunzi," amesema Dkt. Salukele.
Ameongeza kuwa kwa sasa, matumizi ya akili mnemba yanawezesha utekelezaji wa shughuli mbalimbali, hivyo sekta ya elimu ya ufundi stadi itaendelea kunufaika na usaidizi kutoka kwa wataalamu wa China katika kuandaa mitaala inayoendana na mahitaji ya sasa ya soko.
Dkt. Salukele amesema kuwa tayari China ina vyuo vya elimu ya juu na kati vinavyotumia teknolojia ya akili mnemba katika kufundishia, na kubainisha kuwa sera ya elimu ya mwaka 2014 pamoja na maboresho yake ya mwaka 2023 inasisitiza elimu yenye ujuzi.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Elimu ya Mkoa wa Sichuan, Jamhuri ya Watu wa China, Prof. Yu Xiaoqi, amesema kuwa wataendelea kushirikiana na Tanzania katika sekta ya elimu kwa kuandaa mitaala rafiki ya elimu inayolenga kuleta tija kwa taifa.









No comments:
Post a Comment