Na. Jeremiah Mbwambo, Bujumbura - Burundi
Mkurugenzi Mtendaji Prof. Abel Makubi leo ameongoza jopo la madaktari Bingwa wa Hospitali ya Benjamin Mkapa kuwahudumuia wagonjwa waliofika katika kambi ya matibabu inayotolewa nchini Burundi katika Mkoa wa Bujumbura
"Leo ni siku ya nane kuwepo hapa nchini Burundi, tulianzia mkoa wa Gitega na sasa tupo mkoa wa Bujumbura tumeona mwitikio ni mkubwa sana wa wananchi, mimi pamoja na madaktari tutawahudumia wananchi wote mpaka usiku" alisema Prof. Makubi
Ameongeza kuwa wagonjwa wote tuliowafanyia upasuaji Gitega wanaendelea vizuri
"Mtakumbuka tulifanya upasuaji wa wagonjwa 57 mkoani Gitega, wagonjwa wote wanaendelea vizuri na wengi wamesharuhusiwa kuendelea na shughuli zao" alisema Prof. Makubi.
Hospitali ya Benjamin Mkapa imeendelea kujiimarisha katika matibabu ya tiba utalii katika ukanda wa Africa Mashariki, adhima ya Hospitali hii ni kutoa matibabu katika kiwango cha kimataifa.
No comments:
Post a Comment