
SEHEMU ya Waandishi wa habari wakifatilia hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe.Mboni Mhita,(hayupo pichani) wakati akizungumza kuhusu Mafanikio ya Serikali ya awamu ya sita kwa kipindi cha Novemba 2020 hadi April 2025.

SEHEMU ya Waandishi wa habari wakifatilia hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe.Mboni Mhita,(hayupo pichani) wakati akizungumza kuhusu Mafanikio ya Serikali ya awamu ya sita kwa kipindi cha Novemba 2020 hadi April 2025.

SEHEMU ya Waandishi wa habari wakifatilia hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe.Mboni Mhita,(hayupo pichani) wakati akizungumza kuhusu Mafanikio ya Serikali ya awamu ya sita kwa kipindi cha Novemba 2020 hadi April 2025.

MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe.Mboni Mhita,akizungumza na Waandishi wa Habari leo Julai 14,2025 jijini Dodoma kuhusu Mafanikio ya Serikali ya awamu ya sita kwa kipindi cha Novemba 2020 hadi April 2025.
Na Mwandishi Wetu -DODOMA
MKOA wa Shinyanga unaendelea kuchanja mbuga katika kukuza uchumi wa viwanda na biashara, kwa kuimarisha mazingira rafiki ya uwekezaji, ukusanyaji wa mapato, utoaji wa leseni, upimaji wa maeneo ya biashara na utekelezaji wa miradi ya kimkakati yenye kuvutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa huo Mboni Mohamed Mhita, katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita, Mkoa wa Shinyanga umefanikiwa kukusanya zaidi ya shilingi bilioni 150.26 kutoka kwenye vyanzo vya mapato ya ndani ya Halmashauri, vikiwemo ushuru wa bidhaa, mazao, leseni za biashara, na mirabaha ya madini.
Mboni ameeleza hayo leo July 14,2025 Jijini hapa wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo ameeleza kuwa hali hiyo imefanya kuwekeza kwa nguvu kwenye miundombinu ya biashara na viwanda ili kuunga mkono dhamira ya Rais Dkt. Samia ya kuijenga Tanzania ya viwanda.
Aidha amesema katika kipindi hicho Mkoa umetekeleza miradi ya thamani ya bilioni 65.5 kutoka mapato ya ndani kwa ajili ya kuboresha huduma muhimu kama masoko, ofisi, barabara za ndani na maeneo ya uwekezaji.
Kwa upande wa sekta ya viwanda na biashara Mhita amesema Mkoa umepima viwanja 10,658 vya biashara, viwanda na huduma mbalimbali, sawa na asilimia 157 ya lengo,Hati miliki za ardhi zimetolewa kwa zaidi ya wafanyabiashara 20,000 kutoka 10,568 mwaka 2020 huku Hati za kimila zikiongezeka kutoka 816 hadi 4,930 mwaka 2025, hatua inayowezesha wananchi kupata mikopo na mitaji kupitia ardhi.
Amesema leseni za wachimbaji wadogo zimeongezeka kutoka 332 hadi 1,766, ikionyesha uhai wa biashara ya madini ambapo Mapato ya halmashauri kutoka sekta ya madini yamepanda kutoka milioni 745 hadi zaidi ya bilioni 3.3.
"Kwa mara ya kwanza, Mkoa wa Shinyanga ulishiriki Maonesho ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) mwaka 2025, hatua iliyopelekea kutangaza bidhaa, wajasiriamali na fursa zilizopo kwa wawekezaji mbalimbali,
Hii ilikuwa fursa muhimu ya kuitangaza Shinyanga kama kitovu cha biashara na uzalishaji Kanda ya Ziwa," amesema Mhita.
Kuhusu miundombinu ya biashara na viwanda ameeleza kuwa Mradi wa TACTIC umetekelezwa kwa thamani ya zaidi ya bilioni 72.6, ukihusisha ujenzi wa masoko ya kisasa – Soko la Sango (Kahama), Soko la Matunda (Kambarage, Shinyanga),Ujenzi wa stendi kuu mpya – Mbulu na Kizumbi na Barabara za viwandani (Zongomela) na mifereji ya mvua.
Licha ya hayo amezungumzia uboreshaji wa maeneo ya viwanda na huduma katika Manispaa ya Kahama na Shinyanga kuwa katika nishati na uwezeshaji biashara Vijiji vyote 506 sasa vimeunganishwa na umeme; vitongoji 982 kati ya 2,704 tayari vina huduma ya umeme.
Amesema TANESCO imewekeza bilioni 492 kutekeleza miradi ya umeme na miradi 133 ya usambazaji Mitungi ya gesi 6,500 imetolewa ili kuendeleza matumizi ya nishati safi kwa ajili ya biashara ndogo, hasa upishi.
Pia amesema Uwezeshaji wananchi kiuchumi umeimarika ambapo vikundi 1,124 vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu vimepatiwa mikopo ya jumla ya bilioni 8.56 huku Kaya 35,055 zikinufaika na mpango wa kunusuru kaya maskini, ambapo zaidi ya bilioni 59.57 zilitolewa kuendeleza miradi ya kilimo na biashara ndogo.
"Mkoa umesajili wajasiriamali 225 waliopatiwa vitambulisho, wakipata sifa ya kupewa mikopo nafuu kupitia benki ya NMB kwa riba ya asilimia 7 tu, " amefafanua
Kwa mujibu wa Mhita, Mkoa unajipanga kuimarisha zaidi viwanda vidogo na vya kati, kwa kushirikiana na SIDO, VETA na sekta binafsi, huku akiwasihi wawekezaji kuchangamkia fursa zilizopo kwa sasa.
"Shinyanga ni hazina ya biashara, rasilimali na nguvu kazi. Huu ndio muda wa kuwekeza kabla fursa hazijachukuliwa na wengine," alisisitiza kwa msisitizo.
No comments:
Post a Comment