Na Mwandishi Wetu, Mwanza
Viongozi wa klabu za michezo za Wizara, Idara, Wakala za Serikali na Ofisi za Wakuu Mikoa Tanzania, wametakiwa kuwa na ushirikiano wa dhati, ili kufanikisha michezo mahala pa kazi.
Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa shirikisho la michezo hiyo (SHIMIWI), Bw. Daniel Mwalusamba wakati wa kufunga mkutano wa maandalizi ya michezo hiyo uliofanyika Jijini Mwanza, kuanzia tarehe 27 - 31 Julai, 2025 , ambapo amesisitiza ushirikiano kutokana na kuwepo kwa viongozi wa muda mrefu na wengine wapya waliochaguliwa hivi karibuni, ambao watakabidhiwa kundi la watumishi kulisimamia kwa kipindi chote cha mashindano, na kwa kuwa hawana uzoefu itawawia vigumu kuwaongoza.
Halikadhalika, Bw. Mwalusamba amewakumbusha viongozi hao kuhakikisha yale yote waliyoyajadili na kuyapitisha kwa dhati kwenda kuyafanyia kazi, ikiwemo maoni kuhusu kanuni ambazo zitakazotumika kwenye michezo hiyo.
“Hatima ya shirikisho hili kudumu ni kwetu sisi kufanya vizuri
No comments:
Post a Comment