WATENDAJI WAHIMIZWA KUSHIRIKIANA NA VYOMBO KUDHIBITI WAHAMIAJI HARAMU - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Sunday, July 27, 2025

WATENDAJI WAHIMIZWA KUSHIRIKIANA NA VYOMBO KUDHIBITI WAHAMIAJI HARAMU




OR - TAMISEMI


Katibu Tawala Mkoa wa Kilimanjaro Kiseo Yusuph Nzowa ametoa wito kwa maafisa Tarafa na Watendanji wa Kata kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama ili kudhibiti wimbi la uhamiaji haramu katika maeneo yao ya kiutawala.

Katibu tawala Nzowa ametoa agizo hilo wakati alikihitimisha mafunzo ya siku mbili ya maafisa tarafa na watendaji wa kata wapya walioajiriwa kuanzia mwezi Julai, 2024/2025.

Amesema “Kila mtanzania ana jukumu la kuitunza amani tuliyonayo lakini nyinyi viongozi ndiyo kiungo muhimu wa mamlaka nyingine katika serikali yetu, hivyo hili la kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama ni muhimu mno katika kudumisha amani tuliyonayo kwa kudhibiti vitendo vya kihalifu ikiwa ni pamoja na kuwabaini na kuwatolea taarifa wahamiaji haramu”.

Aidha amewataka maafisa hao kulipa kipaumbele suala la ukusanyaji wa mapato ya ndani katika mamlka za serikali za mitaa, ili kuiwezesha serikali kupata nguvu za kiuchumi na kifedha kuendelea kujenga miradi mbaimbali ya maendeleo kama vile hospitali,barabara, shule, umeme na maji.

Mafunzo hayo kwa Maafisa tarafa na watendaji wa kata katika kanda ya kasikazini yamewashirikisha washiriki kutoka mikoa ya Arusha,Tanga, Kilimanjaro na Manyara.






No comments:

Post a Comment