WAZIRI ULEGA AKUTANA NA MTOTO MWENYE KIPAJI CHA UJENZI WA BARABARA NA MADARAJA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Sunday, July 20, 2025

WAZIRI ULEGA AKUTANA NA MTOTO MWENYE KIPAJI CHA UJENZI WA BARABARA NA MADARAJA


Waziri wa Ujenzi Abdallah Ulega amekutana na mtoto Ridhiwani Martin Asheri mwenye umri wa miaka 13 kutoka Kibaigwa mkoani Dodoma, mwenye kipaji cha ujenzi wa madaraja na barabara.

Waziri Ulega amekutana na mtoto huyo Leo tarehe 20, Julai 2025 katika Ofisi ndogo za Wizara hiyo jijini Dar es salaam, na kufanya nae mazungumzo akiwa ameongozana na familia yake.

Baada ya mazungumzo hayo Waziri Ulega ameahidi kumsaidia kijana huyo kuhakikisha anatimiza ndoto zake za kuwa Mhandisi mkubwa hapo baadaye.

Waziri Ulega amesema atakaa na Wizara ya Elimu kuona ni sehemu gani sahihi kijana huyo apelekwe ili kuweza kumsaidia kielimu hasa kwenye maswala ya ujenzi.

Pia Waziri Ulega amemtembeza mtoto huyo katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam ili aweze kujionea kwa macho yale ambayo alikuwa anayatengeneza akiwa nyumbani kwao kwa kuyaona tu kwenye TV.

Miongoni mwa maeneo hayo ni Daraja la Kijazi lililopo Ubungo, Daraja la Tanzanite na kituo cha Treni ya Mwendokasi (SGR) Posta.

No comments:

Post a Comment