WIZARA YA FEDHA YATWAA TUZO MAONESHO YA 49 YA SABASABA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, July 7, 2025

WIZARA YA FEDHA YATWAA TUZO MAONESHO YA 49 YA SABASABA


Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Selemani Jafo (Kulia), akimkabidhi tuzo Afisa Habari Mwandamizi wa Wizara ya Fedha, Bw. Ramadhan Kissimba, baada ya Wizara ya Fedha kuibuka Mshindi wa Tatu wa Jumla kwa upande wa Wizara zilizoshiriki Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam, yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE), katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere, Kilwa Road, Jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya Watumishi wa Wizara ya Fedha wakionesha bashasha katika picha ya pamoja baada ya Wizara hiyo kuibuka Mshindi wa Tatu wa Jumla kwa upande wa Wizara zilizoshiriki Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam, yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE), katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere, Kilwa Road, Jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya Maafisa wandamizi wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Fedha wakiwa katika picha ya pamoja wakisheherekea ushindi wa Wizara hiyo baada ya kuibuka Mshindi wa Tatu wa Jumla kwa upande wa Wizara zilizoshiriki Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam, yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE), katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere, Kilwa Road, Jijini Dar es Salaam.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dar es Salaam)


Na. Peter Haule na Joseph Mahumi,WF, Dar es Salaam


Wizara ya Fedha imeibuka na tuzo ya Mshindi wa Tatu wa jumla kwa upande wa Wizara zilizoshiriki Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (Sabasaba) yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba, Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.

Tuzo hizo zimetolewa na Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Seleman Jaffo ambapo kwa upande wa Wizara ya Fedha Tuzo hiyo imepokelewa na Afisa Habari Mwandamizi, Bw. Ramadhan Kissimba, kwa niaba ya Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Bw. Benny Mwaipaja, ambapo ushindi huo umetokana na Wizara zilizotoa huduma bora kwa wananchi katika Maonesho hayo.

Wizara ya Fedha inatoa huduma katika Maonesho hayo kupitia Idara, Vitengo na Taasisi zilizochini ya Wizara ya Fedha ikiwa ni pamoja na Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), Mfuko wa Dhamana na Uwekezaji Tanzania (UTT AMIS), Mfuko wa Self Microfinance, Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) na Soko la Bidhaa Tanzania (TMX).

Taasisi nyingine ni pamoja na Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), Baraza la Masoko ya Mitaji (CMT), Benki ya Maendeleo TIB na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Hazina SACCOS, Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA), Mamlaka ya Rufaa za Zabuni za Umma (PPAA) na Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA).

No comments:

Post a Comment