DODOMA YAWAKARIBISHA WAWEKEZAJI KATIKA SEKTA YA MADINI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, August 6, 2025

DODOMA YAWAKARIBISHA WAWEKEZAJI KATIKA SEKTA YA MADINI


Na Mwandishi Wetu, Dodoma


Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Dodoma, Mhandisi Menard Msengi, amewakaribisha wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kuwekeza katika Sekta ya Madini, akisisitiza kuwa mkoa wa Dodoma umebarikiwa kuwa na madini ya aina mbalimbali yenye fursa kubwa za kiuchumi.

Akizungumza alipotembelea Banda la Tume ya Madini katika Maonesho ya Kilimo ya Nane Nane yanayoendelea katika Viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma, Mhandisi Msengi amesema ofisi yake imejipanga kikamilifu kutangaza fursa hizo kwa lengo la kuvutia wawekezaji zaidi.

“Dodoma ni miongoni mwa mikoa yenye utajiri mkubwa wa madini mbalimbali hivyo tunawakaribisha wawekezaji kuja kushirikiana nasi kwa maendeleo ya taifa na wananchi,” amesema Mhandisi Msengi.

Maonesho ya Nane Nane yameendelea kuwa jukwaa muhimu kwa wadau wa sekta mbalimbali, ambapo Tume ya Madini inatumia fursa hiyo kutoa elimu kuhusu fursa za uwekezaji katika Sekta ya Madini.









No comments:

Post a Comment