Afisa Uhusiano Mwandamizi, Edwin Mwijage na Afisa Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma, Halima Kambi wakitoa elimu ya mita za malipo kabla (prepaid meter) na kifaa cha kupimia urefu wa kisima kwa wateja waliotembelea Banda la Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) kwenye maonesho ya Wakulima NaneNane katika Viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma Agosti 05, 2025.
DUWASA ni miongoni mwa taasisi za Serikali zinazoshiriki maonesho hayo yaliyoanza Agosti 1 – 8, 2025 na inatoa huduma mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupokea kero na kutatua changamoto zinazohusiana na huduma ya maji na kutoa elimu kwa Wananchi juu ya masuala mbalimbali yanayohusu maji na usafi wa mazingira.


No comments:
Post a Comment