WAKAGUZI WAHIMIZWA UMAKINI NA KASI KATIKA UKAGUZI WA MIRADI YA MAENDELEO - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, December 16, 2025

WAKAGUZI WAHIMIZWA UMAKINI NA KASI KATIKA UKAGUZI WA MIRADI YA MAENDELEO



Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali Msaidizi, Mhandisi Kenneth Nindie, akizungumza jambo wakati wa siku ya pili ya mafunzo ya kuwajengea uwezo Wakuu wa Vitengo vya Ukaguzi na Wakaguzi Wakuu wa Ndani kutoka Wizara, Sekretarieti za Mikoa, Halmashauri na Taasisi mbalimbali za Serikali zaidi ya 90, yaliyoandaliwa na Wizara ya Fedha, katika ukumbi wa Cate Hotel mjini Morogoro, ambapo pamoja na mambo mengine aliwataka Wakaguzi wa Ndani kuongeza kasi, umakini na ubunifu katika kufanya ukaguzi wa miradi ya maendeleo, ili kuhakikisha fedha za umma zinatumika kwa ufanisi, uwazi na kuwa na matokeo chanya kwa wananchi.

Mtaalamu wa masuala ya ukaguzi kutoka Taasisi ya KPMG, Bw. Isaya Tumaini, akieleza jambo kuhusu Viwango vya Utoaji Taarifa za Uendelevu vya ISSB (ISSB Sustainability Reporting Standards), wakati wa siku ya pili ya mafunzo ya kuwajengea uwezo Wakuu wa Vitengo vya Ukaguzi na Wakaguzi Wakuu wa Ndani kutoka Wizara, Sekretarieti za Mikoa, Halmashauri na Taasisi mbalimbali za Serikali zaidi ya 90, yaliyoandaliwa na Wizara ya Fedha, katika ukumbi wa Cate Hotel mjini Morogoro.



Baadhi ya Wakuu wa Vitengo vya Ukaguzi na Wakaguzi Wakuu wa Ndani kutoka Wizara, Sekretarieti za Mikoa, Halmashauri na Taasisi mbalimbali za Serikali zaidi ya 90, wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zinatolewa wakati wa siku ya mafunzo ya kuwajengea uwezo wakaguzi hao, yaliyoandaliwa na Wizara ya Fedha, katika ukumbi wa Cate Hotel mjini Morogoro.

Mkadiriaji Mjenzi Mwandamizi kutoka Idara ya Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali- Wizara ya Fedha, Qs. Justa Justice akieleza jambo kuhusu Thamani ya Fedha (Value for Money - VFM) na Ukaguzi katika miradi ya maendeleo, wakati wa siku ya pili ya mafunzo ya kuwajengea uwezo Wakuu wa Vitengo vya Ukaguzi na Wakaguzi Wakuu wa Ndani kutoka Wizara, Sekretarieti za Mikoa, Halmashauri na Taasisi mbalimbali za Serikali zaidi ya 90, yaliyoandaliwa na Wizara ya Fedha, katika ukumbi wa Cate Hotel mjini Morogoro.

Mhandisi Umeme Mwandamizi kutoka Idara ya Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali- Wizara ya Fedha, Mhandisi Asajile Mwambungu, akieleza jambo kuhusu Uzingatiaji wa Thamani ya Fedha katika Usanifu wa Miradi (Value for Money Consideration in Project Design), wakati wa siku ya pili ya mafunzo ya kuwajengea uwezo Wakuu wa Vitengo vya Ukaguzi na Wakaguzi Wakuu wa Ndani kutoka Wizara, Sekretarieti za Mikoa, Halmashauri na Taasisi mbalimbali za Serikali zaidi ya 90, yaliyoandaliwa na Wizara ya Fedha, katika ukumbi wa Cate Hotel mjini Morogoro.


(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Morogoro)


Na. Joseph Mahumi, Morogoro


Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali Msaidizi, Mhandisi Kenneth Nindie, amewataka Wakaguzi wa Ndani kuongeza kasi, umakini na ubunifu katika kufanya ukaguzi wa miradi ya maendeleo, ili kuhakikisha fedha za umma zinatumika kwa ufanisi, uwazi na kuwa na matokeo chanya kwa wananchi.

Akizungumza katika siku ya pili ya mafunzo ya kuwajengea uwezo Wakuu wa Vitengo vya Ukaguzi na Wakaguzi Wakuu wa Ndani kutoka Wizara, Sekretarieti za Mikoa, Halmashauri na Taasisi mbalimbali za Serikali zaidi ya 90, yaliyoandaliwa na Wizara ya Fedha, yanayoendelea katika ukumbi wa Cate Hotel mjini Morogoro, Mhandisi Nindie alisema Serikali kupitia Wizara ya Fedha itaendelea kuboresha mazingira ya kazi kwa kuendelea kuwajengea uwezo Wakaguzi katika maeneo mengine mapya ya ukaguzi ikiwemo Ukaguzi wa Mazingira, Kijamii na Utawala Bora (Environmental, Social, and Governance-ESG) pamoja na Ukaguzi wa Thamani ya Fedha (Value for Money-VFM).

“Tunataka kuona wakaguzi wa ndani wanakuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha miradi ya maendeleo inaleta thamani halisi ya fedha, inazingatia misingi ya utawala bora na kulinda mazingira kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho, hivyo tutaendela kuwajengea uwezo kwenye maeneo mengine pia tofauti na haya ya ESG na VFM” alisema Mhandisi Nindie.

Aliongeza kuwa mafunzo hayo ni sehemu ya jitihada za Serikali kuhakikisha wakaguzi wa ndani wanakuwa na uelewa wa kina wa masuala mbalimbali ili kuimarisha uwajibikaji na matumizi bora ya rasilimali za umma.

Katika siku ya pili ya mafunzo hayo, wakaguzi walipata fursa ya kujifunza kuhusu Viwango vya Utoaji Taarifa za Uendelevu vya ISSB (ISSB Sustainability Reporting Standards), Mandhari ya Udhibiti na Uzingatiaji wa Kanuni (Regulatory and Compliance Landscape), na Uzingatiaji wa Thamani ya Fedha katika Usanifu wa Miradi (Value for Money Consideration in Project Design).

Mafunzo hayo yanatarajiwa kuongeza uwezo wa wakaguzi katika kufanya kaguzi za miradi miradi ya maendeleo na kuhakikisha fedha za umma zinatumika kwa tija na matokeo endelevu kwa jamii.

No comments:

Post a Comment