DUWASA YAWATAKA WANANCHI KUTUMIA FURSA YA MAONESHO YA NANENANE KUPATA ELIMU YA HUDUMA ZA MAJI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, August 7, 2025

DUWASA YAWATAKA WANANCHI KUTUMIA FURSA YA MAONESHO YA NANENANE KUPATA ELIMU YA HUDUMA ZA MAJI


Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA), Mhandisi Aron Joseph, amewataka wananchi kutumia vyema maonesho ya Nanenane yanayoendelea jijini Dodoma kwa ajili ya kupata huduma na elimu zinazotolewa na taasisi zilizopo chini ya Wizara ya Maji.

Mhandisi Aron ametoa wito huo alipotembelea Banda la Wizara ya Maji, ambapo DUWASA pamoja na taasisi nyingine za wizara hiyo wanaendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu masuala mbalimbali yahusuyo rasilimali ya maji.

Aidha, amewakumbusha wananchi kutambua kuwa huduma ya maji ni msingi wa maendeleo mengi, hivyo ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha huduma hiyo inakuwa endelevu kwa kulipa ankara za maji kwa wakati ili kuwezesha upatikanaji wake kwa uhakika.

Vilevile, Mhandisi Aron amesema wananchi watakaotembelea banda hilo wanaweza kufahamu ratiba ya upatikanaji wa maji katika maeneo yao pamoja na njia mbalimbali za utatuzi wa changamoto zinazowakabili katika sekta ya maji.

Maonesho ya Nanenane mwaka huu yamebeba kaulimbiu isemayo: "Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi 2025."



No comments:

Post a Comment