MTWALE AHIMIZA VIONGOZI KUTUMIA LUGHA YA STAHA KWA WANANCHI NA WATUMISHI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, August 29, 2025

MTWALE AHIMIZA VIONGOZI KUTUMIA LUGHA YA STAHA KWA WANANCHI NA WATUMISHI



Na OR- TAMISEMI


Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – TAMISEMI anayeshughulikia Serikali za Mitaa, Bw. Sospeter Mtwale amewahimiza Wakuu wa Idara na Vitengo wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kutumia lugha ya staha kwa wananchi na watumishi wanaowasimamia pindi wanapowahudumia.

Bw. Mtwale amesema hayo wakati akifungua mafunzo ya Uongozi kwa viongozi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa yalioratibiwa na Ofisi ya Rais – TAMISEMI kwa kushirikiana na Taasisi ya Uongozi (UONGOZI INSTITUTE), ambayo yameanza leo tarehe 29 Agosti, 2025 katika Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Julius Nyerere kilichopo Kibaha mkoani Pwani ambapo amewahimiza viongozi hao kushughulikia malalamiko yanayowasilishwa kwao na watumishi wa ngazi za chini na pamoja na wananchi.

“Mafunzo haya yameandaliwa kwa ajili ya kuwawezesha ninyi Wakuu wa Idara na Vitengo muwe na uwezo wa kiutendaji ambao utawawezesha kutekeleza majukumu yenu kwa ufanisi na uadilifu,” amesisitiza Mtwale.

Katika kusisitiza umuhimu wa uadilifu katika uongozi, Bw. Mtwale amesema mafunzo yanayotolewa yanalenga kuongeza umahili na ujuzi katika utendaji wa kazi ikiwa ni pamoja na kuwajengea uwezo wa kutatua changamoto zinazokwamisha utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.

Kwa upande wake Katibu Tawala wa mkoa wa Pwani, Pili Mnyema amesema mafunzo hayo yatasaidia kuwabadilisha viongozi hao kifikra na kuboresha utendaji kazi wao, hivyo amewasihi viongozi hao kuzingatia mafunzo wanayopewa ili wawe mfano bora wa viongozi wa kuigwa kwa watumishi wanaowasimamia pamoja na jamii inayowazunguka.

No comments:

Post a Comment