NJAMASII CHIWANGA NYOTA YAKE YANG'ARA KATIKA KAMPENI KWA WAJUMBE WA JIMBO LA MPWAPWA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Sunday, August 3, 2025

NJAMASII CHIWANGA NYOTA YAKE YANG'ARA KATIKA KAMPENI KWA WAJUMBE WA JIMBO LA MPWAPWA




Na Barnabas kisengi Mpwapwa


Mbio za kuwania nafasi ya ubunge wa Jimbo la Mpwapwa kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) zinaendelea kushika kasi, baada ya kutangazwa kwa majina ya wagombea saba waliopitishwa na Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi kwa ajili ya kwenda kuomba ridhaa ya Wajumbe wa Chama hicho.

Wagombea hao wameanza kujinadi mbele ya wajumbe wa CCM katika kata mbalimbali za jimbo hilo, wakiainisha dira na mikakati yao ya kuleta maendeleo endapo watapata ridhaa.

Kampeni za ndani ya chama cha Mapinduzi (CCM) zilianza Julai 30, 2025 na zitahitimishwa Agost 3, 2025.

Ambapo Njamasii Chiwanga aliyekuwa mkurugenzi wa Mazingira kutoka kampuni ya Lead foundation (Kisiki hai) wilayani Mpwapwa ni miongoni mwa watia nia saba waliochaguliwa kupeperusha bendara ya CCM katika Jimbo la Mpwapwa.

Katika hotuba yake kwa wajumbe Njamasii Chiwanga ameainisha vipaumbele vyake vinavyolenga kutatua kero za msingi zinazowakabili wananchi wa jimbo hilo, akisisitiza dhamira ya utumishi uliotukuka na ushirikishwaji wa jamii katika maamuzi ya maendeleo.

Njamasii Chiwanga amesema kuwa Wajumbe wakimpatia ridhaa ya kuwa Mbunge wa jimbo la Mpwapwa atahakikisha wanatekeleza vizuri ilani ya Chama cha Mapinduzi katika vipao mbele vilivyopo katika jimbo hilo

" Nitahakikisha ninasimamia utekelezaji wa ilani ya chama cha Mapinduzi ikiwepo mikopo kwa Makundi ya wanawake,vijana,Wazee na makundi ya watu wenye ulemavu"amesema chiwanga

Watia nia saba waliojitokeza kuwania nafasi hiyo ya ubunge katika jimbo la Mpwapwa Njamasii Chiwanga, ni mtoto wa askofu Mstaafu wa kanisa la Anglican na Baba yake pia aliwahi kuhudumu kama Waziri wa elimu katika kipindi cha uongozi wa Serikali ya awamu ya kwanza na pili.

Mbio hizo za kusaka kura za maoni zinahitimishwa leo Jumapili na kesho Agost 4 kutafanyika zoezi la kupigwa kura za maoni za chama cha Mapinduzi.




No comments:

Post a Comment