POLISI DODOMA YAWAHUDUMIA WANANCHI KUPITIA KAMBI YA MATIBABU YA AFYA CHECK FOUNDATION - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, August 14, 2025

POLISI DODOMA YAWAHUDUMIA WANANCHI KUPITIA KAMBI YA MATIBABU YA AFYA CHECK FOUNDATION



Afisa Mnadhimu wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (ACP) William Mwamafupa ameongoza uzinduzi wa kambi maalum ya matibabu katika Kituo cha Afya cha Polisi Dodoma, ikihusisha wataalamu kutoka Hospitali ya Benjamin Mkapa na Kituo cha Afya cha Polisi.

Huduma hizo zinazotolewa bure kwa askari, familia zao na wananchi, ni sehemu ya ushirikiano baina ya Jeshi la Polisi na taasisi ya *Afya Check Foundation*, kwa lengo la kuimarisha afya za wananchi na watendaji wa vyombo vya ulinzi.

Kwa mujibu wa Dkt. Jackson Shoo, Mkuu wa Kituo cha Afya cha Polisi, huduma zinazotolewa ni pamoja na matibabu ya magonjwa ya dharura, uchunguzi wa afya ya moyo na huduma nyingine za tiba.

Mtaalamu kutoka Hospitali ya Benjamin Mkapa amepongeza ushirikiano huo na kueleza kuwa hadi sasa zaidi ya wagonjwa 60 wamehudumiwa.

Kambi hiyo ya matibabu itaendelea hadi Agosti 18, 2025, na iko wazi kwa wananchi wote wanaohitaji huduma.





No comments:

Post a Comment